JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Mabiti azingatie onyo la wananchi wa Simiyu

Machi 28, mwaka huu wananchi wa Simiyu walimtahadharisha Mkuu wa Mkoa huo, Paschal Mabiti, dhidi ya genge la wafanyabiashara wakubwa wa pamba, vinginevyo “watamuweka mfukoni”. Mabiti aliyeteuliwa hivi karibuni kushika nafasi hiyo na kupangiwa kwenda huko, alikuwa Mkuu wa Wilaya…

Huyu ndiye Kanumba niliyemfahamu

Kulikuwa na vilio na simanzi Mtaa wa Vatican, Sinza Dar es Salaam, nyumbani kwa aliyekuwa mwigizaji maarufu ndani na nje ya Tanzania, Steven Charles Kanumba ‘The Great’. Kanumba alifariki dunia alfajiri ya kuamkia Aprili 7, mwaka huu.

Kimbembe cha petroli London kama Dar

Wakati Jiji la Dar es Salaam lilipokumbwa na zahama ya ukosefu wa mafuta na vurugu kwenye vituo vya petroli na dizeli, sote tulibaki vinywa wazi.

‘Ushindi wa Nassari ni hukumu kwa mafisadi’

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema ushindi wa Joshua Nassari katika Jimbo la Arumeru Mashariki, ni hukumu mpya ya vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na viongozi wa Serikali.

Mpimeni Zitto kujua endapo anatosha kuwa Rais au hatufai

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara, Zitto Zuberi Kabwe, ametangaza rasmi nia yake ya kutaka kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Ukombozi wa taifa umeanzia Arumeru

Pole Sioi Sumary. Hongera Joshua Nassari. Nyota ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inachanua. CCM waanze kujifunza kuwa kambi rasmi ya upinzani mwaka 2015.
[caption id="attachment_2" align="alignleft" width="158"]Deodatus BalileDeodatus Balile[/caption]
Haya ni maneno ya utangulizi niliyolazimika kuanza nayo katika safu hii ya Sitanii. Ikiwa mazingira hayatabadilika, nitakachokitabiri hapa ndicho kitakachotokea mwaka 2015.