JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Dar es Salaam ina viongozi wabovu sijapata kuona

Wiki hii jicho langu limekutana na kitu kinachoitwa mipango miji. Nimejipa muda wa kufikiri na kulinganisha matamanio yetu kama Watanzania juu ya tunachokiita miji safi na bora iliyopangiliwa. Ulinganisho huu nimeufanya ndani na nje ya nchi. Nimejaribu kuangalia miji ya mikoa kama Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera na Dar es Salaam.

Uncle Tom naye atafukuzwa Yanga kama Timbe au Papic?

Msimu uliopita, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) yenye makao yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini iliyokuwa ikitetea ubingwa wake, ilifundishwa na makocha watatu kwa nyakati tofauti. Kwanza ilianza ligi hiyo, Agosti mwaka jana ikiwa na Sam Timbe, Mganda…

Kwa dhuluma hii nchi haitatulia

 

Ndugu msomaji, tazama picha iliyo katika ukurasa huu, kisha utafakari. Nimeitumia kama kielelezo halisi cha kutusaidia kuibua mjadala wa maana kuhusu hatima ya umasikini unaowaandama watoto wa masikini katika Taifa letu.

 

January Makamba amefanya jambo la kuigwa

Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba, ametangaza kuwa amejipanga kuongeza kasi ya maendeleo ya elimu katika jimbo hilo, kazi itakayofanyika kwa kupitia Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) kuanzia mwaka huu.

 

Programu hiyo itagharimu Sh. milioni 40 ikijumuisha vivutio kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari; yote ikilenga kuongeza tija na umakini wa kujifunza na kusaidia juhudi zinazofanywa na serikali katika elimu.

Ardhi ya Tanzania inavyoporwa na matajiri matapeli

*Kambi ya Upinzani yaanika bungeni uozo wa kutisha

*Familia ya Chavda yavuna mabilioni na kutokomea

 

Hii ni sehemu ya hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee, aliyoitoa bungeni wiki iliyopita, akieleza namna ardhi ya Tanzania inavyohodhiwa na wafanyabiashara na matajiri matapeli…


MASHAMBA YALIYOBINAFSISHWA AMBAYO HAYAJAENDELEZWA

Mheshimiwa Spika, wakati akihitimisha bajeti ya ardhi mwaka jana, Waziri wa Ardhi aliliahidi Bunge lako Tukufu kwamba baada ya Bunge la bajeti wizara ingekwenda kufanya ukaguzi huru wa nani ametelekeza mashamba. Alisisitiza kwamba wawekezaji wote waliotelekeza mashamba “the honeymoon is over.”

Sinema kwa wasioona zaja

  Badala ya utaratibu wa zamani sasa waonyesha sinema wamebuni utaratibu mpya wenye kuwawezesha watu wasioona kuangalia sinema sambamba na watu wanaoona.   Teknolojia hii ya aina yake, iko sawa na zile zinazotumika kwenye ndege ikiwa angani, ambapo mtu anaweza…