JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Niliyojifunza ufunguzi wa Olimpiki

JIJI hili sasa hivi hakuna kingine kinachozugumzwa wala kusikilizwa kupita michezo ya Olimpiki. Nimekubali kwamba ni michezo mikubwa na faida yake kwa waandaaaji si ndogo.

Ukishaona watu wanafanya kampeni kubwa kama Uingereza ili tu waandae kitu hiki kwa mara ya tatu, lazima ujue kuna manufaa.

Bahanuzi aleta ladha katika soka

LICHA ya Tanzania kumudu kulibakiza nyumbani Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati – maarufu zaidi kwa jina la Kagame – mshambuliaji wa Simba Sports Club, Felix Mumba Sunzu ameibuka kuwa galasa huku mashabiki wakijiuliza kuhusu sifa zinazofanya timu hiyo iendelee kumng’ang’ania.

Danadana za Sheria ya Habari zitaisha lini?

Wiki iliyopita Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, amewasilisha bajeti ya wizara yake kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma. Si nia yangu kujadili bajeti hii inayofikia wastani wa Sh bilioni 19. Na wala sitajadili danadana ilizopigwa bajeti hii, ambayo awali ilikuwa iwasilishwe Julai 18, lakini kwa mshangao ikasogezwa ghafla hadi Agosti 7, kisha kinyemela ikarejeshwa Julai 24.

Uzalendo: Mtihani wa kuwa raia

Huwa kila jamii yenye kujiheshimu hujiwekea vigezo vya watu wanaotakiwa kuwa ndani yake. Mataifa nayo – kwa kuwa yana mipaka yake yana watu ambao ruksa kuwa ndani – na wengine wote haruhusiwa kuingia, kukaa kwa muda mfupi au mrefu hadi kwa ruhusa maalumu (viza).

JKT ya wiki 3 kwa wabunge ni utani

Machi 17 mwakani imepangwa kuwa tarehe ya kurejesha upya mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa mujibu wa sheria ambayo Serikali iliyafuta mwaka 1992.

Kilichonisikitisha ajali ya meli Zanzibar

Wiki iliyopita kwa mara nyingine taifa letu limeshuhudia majonzi ya aina yake baada ya Watanzania wengine wapatao 150 kupoteza maisha baada ya meli waliyokuwa wakisafiria kuzama.