JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Muungano ndiyo mboni ya Tanzania (2)

Kwa akili za kawaida kabisa, mtu unajiuliza kwani huo uislamu au ukabila umejikita katika mkoa wa mjini magharibi tu? Kwani Zanzibar na Pemba ni mkoa huo huo mmoja tu? Mbona kiserikali tunajua iko mikoa mitano Visiwani? Mjini Magharibi, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja kuna Chakechake kule Pemba na Mkoani kule Kusini Pemba ?

Watanzania tuache woga kudai haki

  Wiki mbili zilizopita, niliamua kubadili utaratibu wa kutumia usafiri wa daladala, nikachagua kutumia gari moshi (treni) kwenda kazini na kurudi nyumbani jijini Dar es Salaam.   Siku moja, takriban dakika nne baada ya kuondoka kituo cha Ubungo Maziwa kuelekea…

Mauaji yanauchafua mkoa wa Mara

Mauji ya raia wasiokuwa na hatia yanaendelea mkoani Mara. Kwa miaka mingi Wilaya ya Tarime ndiyo iliyosifika kwa vitendo hivyo.

Sarafu moja Afrika Mashariki ni mtego – 2

Wiki iliyopita niliandika juu ya hatari ya kuanzishwa kwa sarafu moja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kukamilisha matakwa ya msingi yenye kujenga mfumo wa kuwezesha sarafu moja kufanya kazi kwa ufanisi. Nilieleza mambo mengi yanayohitaji kufanyika kabla ya kufikia uamuzi wa kuanzisha sarafu moja au la.

Yah: Kama ningekuwa waziri wa wawekezaji na ajira

Wanangu, nianze kwa kuwapa hongera ya Krismasi na kwamba mliofanikiwa kufika katika Sikukuu hii, hamna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani si wote waliopata bahati hii ambayo ninyi kwa nafasi na upendeleo wa nafsi zenu kwa Mwenyezi Mungu mmefanikiwa.

Msajili Hazina avunja sheria

*Adai kusaidiana na Waziri Mkuu kutoa uamuzi

*Aonesha dharau kwa Bunge, Waziri kufafanua

 

Msajili wa Hazina, Elipina Mlaki, ameendelea kukiuka sheria, maagizo ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa kulazimisha kuhudhuria vikao vya Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma nchini.