JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Nchi inavyoliwa

[caption id="attachment_695" align="alignleft" width="266"]Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa[/caption]Raia wa Uswisi, Dk. George Hess, anatuhumiwa kujimilikisha na kuuza ardhi ya ufukwe wa Amboni uliopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, kinyume cha sheria. Dk. Hess, anayeishi nchini Kenya, kupitia tovuti yake ya ambonibeach.com, amejitangazia ‘Jamhuri’ katika eneo hilo, kuwa ndiye mmiliki pekee Tanzania mwenye ufukwe, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999.

Sheria ya Mipango Miji namba 7 ya mwaka 2008 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, inakataza mtu yeyote kumiliki ufukwe wa bahari bali fukwe zinapaswa kumilikiwa na umma. Lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha fukwe hazihatarishi amani, ulinzi na usalama wa raia.

RATIBA YA MASHINDANO YA UEFA

Jumanne Februari 19, 2013 MUDA TIMU UWANJA 4:45 usiku Arsenal vs Bayern Munich Emirates 4:45 usiku FC Porto vs Malaga Dragao Jumatano Februari 20, 2013 4:45 usiku AC Milan vs Barcelona Giuseppe Meazza 4:45 usiku Galatasaray vs Schalke 04 Turk…

Wambura: Uongozi mbovu unaua soka Tanzania

Mdau maarufu wa soka nchini, Michael Wambura (pichani kulia), amekosoa soka la Tanzania kwamba linadumazwa na uongozi mbovu.

Yah: Sasa naomba nimchague rais

Nianze kwa kuomba radhi kwa kutoonekana wiki jana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, nia ni moja na tuko pamoja katika kufanikisha mambo muhimu kwa jamii yetu iliyoparaganyika kimaadili, kisiasa na kiuchumi.

Nchi ya usingizi na wapiga soga

Anaweza kuwa na upungufu wake, lakini ni ukweli kwamba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ni mmoja wa viongozi wenye uamuzi na mbinu zinazoleta nuru ya kuwapo mabadiliko katika utendaji kazi miongoni mwa watumishi wa umma.

FASIHI FASAHA

Kuchinja nyama ni sababu ya kufarakana?

Sikilizeni maneno, wasanii tunayosema, jiepusheni navyo vitendo vitakavyotutenganisha, kufarakana, kuchukiana kumeshaanza, kukamiana kutukanana sasa ni sera, Watanzania kuweni macho, Taifa linakwenda pabaya tutakuja jijutia.