JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Sasa tusichezee tena madaktari

Ulimwengu wa mtandao ni kitu kizuri sana. Watu wanawasiliana kwa masafa marefu katika muda mfupi kabisa. Wazungu walikuwa wanasema nasi tukawa tunashangaa, lakini nasi tunaitikia leo kiukweli kweli, kwamba dunia imekuwa kijiji.

Ukombozi wa taifa umeanzia Arumeru

[caption id="attachment_2" align="alignleft" width="158"]Deodatus BalileDeodatus Balile[/caption]Pole Sioi Sumary. Hongera Joshua Nassari. Nyota ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inachanua. CCM waanze kujifunza kuwa kambi rasmi ya upinzani mwaka 2015. Haya ni maneno ya utangulizi niliyolazimika kuanza nayo katika safu hii ya Sitanii. Ikiwa mazingira hayatabadilika, nitakachokitabiri hapa ndicho kitakachotokea mwaka 2015.

Mwaka 1929 kilipoanzishwa chama cha Tanzania African Association (TAA), lengo lao ambalo lilikuja kuchukuliwa na Tanganyika African Union (TANU) mwaka 1957, lilikuwa ni jinsi ya kuondokana na unyanyasaji wa mkoloni. Unyanyasaji unaozungumzwa hapa ni pamoja na yaliyokuwa yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.

Nassari amgaragaza Sioi kwa kura zaidi ya 7,000

Nape akubali kushindwa, aipongeza Chadema
Sasa ni chereko, shangwe kila mahali nchini

Mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari, amembwaga mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki. Kutangazwa kwa Nassari kuwa mshindi wa kiti hicho, kumeibua shamrashamra si Arumeru pekee, bali ndani ya nje ya nchi, hasa kwa wapenda mageuzi.