Category: MCHANGANYIKO
Habari sahihi zina nguvu kuliko bunduki
Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa kwenye harakati za kuhakikisha nchi yetu inatambua uhuru wa vyombo vya habari, haki ya kupata habari na uhuru wa kutoa mawazo. Harakati hizi zimenifikisha hatua ya kufahamu kwa kina umuhimu wa habari na hasa habari sahihi.
Udhibiti maegesho holela Temeke, changamoto zake
Jiji la Dar es Salaam ni moja ya majiji yanayoongoza kwa idadi kubwa ya wakazi hapa nchini. Hali hiyo inasababishwa na ongezeko la watu wanaoingia jijini kila kukicha, wakitokea mikoa mingine katika harakati za kutafuta maisha bora, ambayo wengi wao wanaamini kuwa yanaweza kupatikana Dar es Salaam.
Mr. Nice kujipanga upya
Soko la muziki wa Tanzania linakua siku hadi siku. Dalili za kukua kwa muziki zinadhihirishwa na ongezeko la wasanii wanaoibuka mara kwa mara. Hali hii imewafanya wasanii wakongwe na waliopata kuwika katika muziki kwa kiasi kikubwa, kufikiria kujipanga upya ili kuendana na soko la kisasa.
Shambulio la Westgate kuahirisha magongo
Mashindano ya magongo kwa mataifa ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamisi wiki hii mjini Nairobi, huenda yakaahirishwa kutokana na mkasa wa shambulio la jengo la kitegauchumi la Westgate lililovamiwa na magaidi wa Al Shabaab.
Usahihi kuhusu Shelutete
Katika toleo lililopita la Septemba 24-30, 2013 kwenye ukurasa huu, kulikuwa na barua iliyoeleza ufisadi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
TEODENSIA MBUNDA
Mwanamke pekee msaidizi wa waziri
Ni asubuhi na mapema siku ya Jumatano napata wazo la kuonana na Msaidizi wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Teodensia Mbunda.