Category: MCHANGANYIKO
Real Madrid kuivua ubingwa Bayern leo
Miamba minne ya soka barani Ulaya, wiki hii inajitupa tena katika viwanja viwili tofauti kucheza nusu fainali ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Miamba hiyo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, vijana wa Pep Guardiola wa Bayern Munich,…
CCM inapohusishwa na kila kitu
Katika maisha ya jadi niliyoishi kijijini, kila kitu kilichotokea kilihusishwa na Mungu. Kama kuku hawakutaga mayai mengi kutokana na kutopewa chakula cha kutosha, watu walisema ni amri ya Mungu.
Kama mtu alikufa kwa ugonjwa kwa sababu ya kucheleweshwa kupelekwa hospitali, watu walisema ni amri ya Mungu. Na kama watoto walichezea moto ukaunguza nyumba, watu walisema ni amri ya Mungu.
Mipasho Bunge la Katiba ikomeshwe
Bunge Maalum la Katiba limeahirisha vikao vyake hadi Agosti mwaka huu, kupisha vikao vya Bunge la Bajeti vitakavyopokea na kujadili taarifa za mapato na matumizi ya Serikali ya Muungano kwa mwaka 2014/2015.
Bunge hilo kabla ya kuahirishwa Aprili 25, mwaka huu kwa takriban miezi miwili, yaani tangu Februari 18, mwaka huu wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba walikuwa katika vikao vizito, wakifanya mambo makuu mawili. Watanzania tumeshuhudia.
IGP Mangu dhibiti udhaifu huu
Katika siku za karibuni, Jeshi la Polisi Tanzania limechukua hatua mbalimbali za kujisafisha mbele ya umma. Ni baada ya kubaini kwamba wananchi wengi walikuwa hawaridhiki na utendaji wa chombo hiki cha dola.
Yah: Litakuwa Taifa la watoto, wazee
Nianze kwa kuwapongeza kutimiza miaka makumi kadhaa ya Muungano, yaani Muungano ambao leo mnadai kuwa una kero ambazo sisi wakati tukiungana tuliona siyo kero za Muungano bali ni chachu za Muungano, na ndizo zinazofanya utamu wa Muungano kuwapo. Sina hakika,…
Nyalandu aweweseka siri kuvuja
*Aanza kuwasaka wabaya wake, awatisha Aprili 22, mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na baadhi ya watendaji waandamizi wa Wizara hiyo mjini Dodoma, alitoa vitisho akiahidi kuwashughulikia wote aliodai kuwa wanavujisha siri za ofisi kwa watu…