JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

CCM ni kama wameitwa na chunusi

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) mwanzoni mwa mkutano wa Bunge unaoendelea sasa, alizungumza maneno ya hekima.

 

Akieleza safari ya kifo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) alifananisha hali hiyo na tajiri anayefilisika. Akasema tajiri anayefilisika huwa hajitambui, na kwamba akijitambua kuwa anafilisika, kamwe hatafilisika. Hatafilisika kwa sababu atajitahidi kutafuta mbinu za kujikwamua. Akasema kwa hali ya mambo ilivyo, CCM haijitambui kama inakufa, na kwa sababu hiyo, inakufa!

Yah: Haiwezekani Mtanzania abaguliwe ndani ya Tanzania

Wanangu, naamini mu bukheri wa afya na mnaendelea kufanya kazi kwa bidii kama tulivyokuwa tukifaya sisi wakati wa ujana na afya zetu.

Yah: Tulianza kusimama dede sasa tunabebwa.

Wanangu nianze kwa kuwapa kongole kwa kazi za kuliendeleza taifa ambalo linamkosi mkubwa na jambo linaloitwa maendeleo, linamkosi kwa sababu kwa kipindi cha miaka hamsini ya tangu kuzaliwa kwake bado linachechemea, kwa ufupi ndio kwanza linaanza kusimama dede ili lipige hatua ya kwanza lakini dalili zote za kushindwa zinajidhihirisha.

Dar es Salaam ina viongozi wabovu sijapata kuona

Wiki hii jicho langu limekutana na kitu kinachoitwa mipango miji. Nimejipa muda wa kufikiri na kulinganisha matamanio yetu kama Watanzania juu ya tunachokiita miji safi na bora iliyopangiliwa. Ulinganisho huu nimeufanya ndani na nje ya nchi. Nimejaribu kuangalia miji ya mikoa kama Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera na Dar es Salaam.

Uncle Tom naye atafukuzwa Yanga kama Timbe au Papic?

Msimu uliopita, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) yenye makao yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini iliyokuwa ikitetea ubingwa wake, ilifundishwa na makocha watatu kwa nyakati tofauti. Kwanza ilianza ligi hiyo, Agosti mwaka jana ikiwa na Sam Timbe, Mganda…

Kwa dhuluma hii nchi haitatulia

 

Ndugu msomaji, tazama picha iliyo katika ukurasa huu, kisha utafakari. Nimeitumia kama kielelezo halisi cha kutusaidia kuibua mjadala wa maana kuhusu hatima ya umasikini unaowaandama watoto wa masikini katika Taifa letu.