JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Bunge lisiposema, wabunge watasema

 

Nimemsikiliza Naibu Spika Job Ndugai akilalamika kwamba nidhamu ya baadhi ya wabunge, hasa vijana si nzuri. Ndugai anarejea matukio kadhaa yaliyotokea wakati wa Mkutano wa Bunge ulioahirishwa wiki iliyopita. Alikwenda mbali zaidi kwa kukumbuka mambo yalivyo tangu kuanza kwa Bunge la Kumi. Analalamika kwamba asilimia zaidi ya 70 ya wabunge wa sasa ni wageni. Kuna vijana wengi ambao bado hawajazisoma na kuzitambua vema Kanuni za Kudumu za Bunge.

Buriani Mbogora, bado sisi tunahangaika na Malawi

 

Moyoni nina majonzi. Natumia neno hili kwa vile siamini macho yangu, lakini ndivyo ilivyo. Hili linatokana na kifo cha mwanahabari mwandamizi, Alfred Mbogora. Nilimwona Mbogora siku moja kabla ya kifo chake, lakini zamu hii hakuwa akifahamu kama nilifika kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini angalau alitikisa mkono na mguu nilipoingia wodini. Hii ilikuwa Ijumaa.

Mahakama imekalia haki yangu miaka 16

Mhariri wa JAMHURI nimevutiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kusoma toleo lenu Na 39 la Agosti 14-20, 2012 lililoongozwa na habari yenye kichwa kisemacho ‘Majaji Vihiyo Watajwa’. Mara tu niliposoma habari hii, nikaona ni vyema nifunge safari na kuja hapo ofisini kwako nieleze kilio changu. Wengi wa majaji waliotajwa wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukandamiza haki yangu.

Hongera Mkapa, Kikwete alijiandalia aibu ya Mahalu

Napata wakati mgumu. Napata shida jinsi ya kuanza makaha haya. Napata shida si kwa sababu nina maslahi binafsi, bali kwa sababu nakumbuka hadithi ya mwanafunzi aliyebeba upodo huku akijifunza kurusha mishale ya sumu. Hakuwa mahiri na hakujua jinsi ya kuvuta upinde. Kwa kicheko kikubwa, aliipaka sumu ncha ya mshale, upinde akauelekeza karibu na tumbo lake, kamba ya kurushia mshale ikatokea mbele yake.

Ni aibu TFF, ZFA kugombea Sh milioni 12 za mgawo wa BancABC

Wiki iliyopita, Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) lililazimika kuutolea ufafanuzi mvutano wa mgawo wa fedha za michuano ya BancABC Super 8 kati yake na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), kilipotishia kuziondoa timu zake. Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa fedha zote zilizotolewa na wadhamini wa michuano hiyo – BancABC – zimelipwa kila sehemu kunakohusika zikiwamo timu zote zinazoshiriki, viwanja vinavyotumika, miji inakochezwa na promosheni ya masoko iliyogharimu shilingi milioni nane.

Olimpiki: Kweli kupanga ni kuchagua

Leo nimeazima busara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema kwamba kupanga ni kuchagua.

Uongozi wa Mwalimu Nyerere haujapata kutokea, si Tanzania tu bali katika nchi nyingi za dunia, hata kama katika hili kuna wale wasioambilika. Kama mipango yote aliyokuwa ameisuka na kuanza kutekeleza Mwalimu ingepata wasimamiaji wazuri, nakuapia leo tungeweza hata kuandaa michezo ya Olimpiki.