Category: MCHANGANYIKO
Demokrasia imepanuka na sasa imevuka mipaka
Oktoba 17 mwaka huu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete atapokea tuzo nchini Uholanzi, barani Ulaya. Ni tuzo inayotokana na kuiwezesha nchi yake kushika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kushamiri demokrasia. Hiyo nchi yake ni Tanzania.
Kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza kwa kushamiri demokrasia barani Afrika hakuna anayeweza kuhoji. Na hakuna anayeweza kudai kwa haki kwamba Wazungu wametumia upendeleo katika kumpa tuzo hiyo. Sisi sote ni mashahidi. Tanzania ni nchi ya demokrasia halisi.
Heri TBS imeamua kuanika hatari ya vilainishi hivi 15
Hivi karibuni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilipiga marufuku kuuzwa kwa vilainishi vya magari na mitambo kutokana na baadhi kutokidhi viwango.
Vipigo vya polisi kwa waandishi vinadhalilisha tasnia ya habari
Kwanza naomba nianze kwa kuwapa pole waandishi wa habari wote waliokutana na zahama ya kipigo kutoka polisi wakati wakitekeleza majukumu yao halali.
Ni majukumu yaliyoandikwa na Katiba ya nchi ya kutafuta habari ili waweze kuuhabarisha umma, ndani na nje ya nchi. Ni tukio lililojiri siku za hivi karibuni.
Profesa Mkumbo uko sahihi, Lowassa jembe
Hivi karibuni, nilipigiwa simu na msomaji wa makala zangu na kuniuliza kama niliwahi kupitia moja ya makala zilizoandikwa na Profesa Kitila Mkumbo, kwenye moja ya magazeti yanayochapishwa hapa nchini. Makala hiyo ilibeba kichwa cha habari kisemacho ‘Msingi na uhalisia wa taswira ya uchapa kazi ya Lowassa’ ya Septemba 24, mwaka huu.
Mrema ni mtu hatari sana — Leo Lwekamwa
*Asema aliwahi kuitosa TLP dakika za mwisho na kuhamia NCCR-Mageuzi
*Mwanzo ilikuwa ahamie Chadema, Mtei akamkatalia akijua…
*Adai ana mipango ya Serikali
* Aamua kurudi CCM kujisalimisha