JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Kuchinja si tatizo, tatizo ni udini

Wiki hii nimelazimika kuandika tena mada hii. Nimeiandika mada hii baada ya kuona moto unazidi kusambaa nchi nzima. Tatizo lilianzia Kanda ya Ziwa kwenye mikoa ya Mwanza na Geita, likaenda Shinyanga, lakini sasa limehamia Tunduma.

Mjue vizuri Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Aprili 13, mwaka 1922, safari ndefu ya maisha ya Mwalimu Kambarage Nyerere iliyochukua miaka 77 na miezi 6 ilianza Mwitongo kijijini Butiama, kilomita takribani 30 kutoka mji wa Musoma, mashariki mwa Ziwa Victoria lililoko kaskazini mwa Tanzania. Siku hiyo mvua kubwa ilinyesha. Mama Mgaya Nyang’ombe, aliyekuwa mke wa tano kati ya 23 wa Chifu Nyerere Burito wa Zanaki, alijifungua mwanae wa pili. Kwa desturi za kabila la Wazanaki, mtoto wa kike ama wa kiume aliyezaliwa siku ya mvua alipewa jina la KAMBARAGE (mzimu wa mvua).

Alliance hiyooo Uingereza

 

Timu ya soka ya Alliance ya jijini Mwanza, imealikwa kushiriki mashindano ya kimataifa yanayojulikana kama International English Super Cup 2013, huku ikiahidi kurejea nchini na ushindi.

Yah: Watekaji wasajiliwe, walipe kodi

Kuna wakati nahisi kama nchi yetu tunahitaji kuwa na ofisi za kijasusi, ambazo zimesajiliwa na zinalipa kodi kuliongezea Taifa mapato.

Nashauri kwa hili waanze na Pinda

Haraka haraka baada ya kuanguka kwa jengo lenye ghorofa 16 katika Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, viongozi wa Serikali wakatoa amri ya kukamatwa kwa Mkandarasi, Mhandisi Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Ukaguzi wa Majengo wa Manispaa ya Ilala.

FASIHI FASAHA

Ulimi mzuri utaimarisha uchumi Tanzania

Juma lililopita nilizungumzia thamani ya faraka ya matumizi ya ulimi wa mwanadamu. Ukitumika vizuri huleta rutuba chanya ya  maendeleo, na ukitumika vibaya huleta rutuba hasi ya maendeleo, iwe ya mtu kikundi cha watu ama Taifa.