JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

FC Lupopo yasifu wachezaji wa Tanzania

*Huenda Kaseja akasajiliwa huko

Katika hali inayoonesha kuwa wanandiga wa Kitanzania wanaosakata kabumbu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanakubalika, Klabu ya Soka ya FC Lupopo imesema wachezaji kutoka Tanzania wanapendwa nchini humo kutokana na uwezo wao kisoka.

Tenisi wajihami Afrika Mashariki, Kati

Timu ya Taifa ya Tenisi inayoshiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15, imeondoka leo kwenda Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ikiwa na matumaini ya kushinda.

Kodi ya simu inarejesha ‘Kodi ya Kichwa’

Taifa letu lipo katika mtikisiko mkubwa. Kuna mjadala mkubwa unaoendelea juu ya uanzishwaji wa kodi ya kumiliki simu. Kodi hii inatajwa na wengi kuwa ni kama kodi ya ‘Kichwa’ iliyobatizwa jina la kodi ya maendeleo baada ya Uhuru.

Tanzania imefikia kilele katika dawa za kulevya

Dawa za kulevya zinazidi kuchafua jina la Tanzania. Zimekuwapo taarifa za orodha ya watu wanaotumia au kuuza dawa hizo hapa nchini, lakini kadri siku zinavyopita tatizo linazidi kuwa kubwa kwa kiwango cha kutisha. Katika hali isiyo ya kawaida, Mtanzania aliyeko kifungoni nchini China ameamua kuanika ukweli wa kinachoendelea Tanzania.

Maghoba: Tanzania isipuuze vitisho vya Kagame

Mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Frank Maghoba, ameitahadharisha Tanzania, akiitaka kutopuuza kauli ya vitisho inayodaiwa kutolewa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, dhidi ya Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Tume ya Katiba inataka kutudhulumu?

Mhariri,

Mimi ninaitwa Issa Juma Dang’ada, ninaishi mjini Nzega, mkoani Tabora. Ni Mjumbe wa Baraza la Katiba Wilaya ya Nzega.