JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Dola yatuhumiwa kwa mauaji Tabora

Kumekuwa na matukio ya mauaji ya watu mara kwa mara katika wilaya za Urambo na Kaliua mkoani Tabora, yanayofanywa na baadhi ya watendaji wa vyombo vya dola, hali inayoendelea kutishia maisha ya watu, huku ikionesha kuwa hakuna hatua za kuridhisha zinazochukuliwa kukabili tatizo hilo.

Wanahangaikia urais 2015, TAMWA waokoe wanawake mkoani Dodoma

Nchi yetu kwa sasa imegeuka taifa la uchaguzi. Ukipita kwenye vijiwe vya kahawa, makao makuu ya vyama vya siasa, na hata hii Katiba mpya inayoandaliwa kila mtu analenga uchaguzi mwaka 2015. Tanzania ni nchi pekee kati ya nchi ninazozifahamu duniani, iliyojenga utamaduni wa kumaliza uchaguzi wanasiasa wakaanza harakati za uchaguzi unaofuata miaka mitano ijayo.

Yah: Kama mimi ningelikuwa Manumba ama wasaidizi wake?

Sasa hivi napenda nikiri wazi kwamba kama kuna mtu ama wana wakati mgumu wa kuingalia rediocall ama kusikilizi simu zao za mikononi za kikazi na siyo kindugu ama urafiki hawana muda wa kuangalia televisheni na kusikiliza redio basi ni kundi zima la Manumba mwenyewe na hao RCO wake wote, poleni lakini ndio kazi mliochagua kutokana na masomo yenu.

Dogo Aslay afurahia maisha ya muziki

Staa wa Bongo katika muziki wa kizazi kipya Aslay Isiaka, ‘Dogo Asley’ ambaye makazi yake ni jijini Dar es Salaam amesema kuwa sasa anfurahia maisha ya muziki kutokana na maendeleo aliyoyapata.

Madee – Nidhamu siri ya mafanikio

Msanii maarufu wa wa muziki nchini, Hamad Ally, maarufu kama  ‘Madee’  (pichani) kutoka katika kundi la Tip Top Connection la Manzese, jijini Dar es Salaam,  amesema kuwa siri ya mafanikio yake katika muziki ni nidhamu.

Mechi klabu bingwa Ulaya kuendelea leo

Wapenzi wa kandanda la Ulaya leo watakuwa na wakati mzuri wa kushuhudia mechi kadhaa za michuano ya soka klabu Bingwa barani Ulaya zikichezwa katika viwanja mbalimbali barani humo.