JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Samata, Ulimwengu kuibeba ‘Kili’ Chalenji

Wachezaji wa TP Mazembe (DRC), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wametajwa kuwa ndiyo wachezaji watakaongoza Jahazi la timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, kutwaa Kombe la Chalenji mwaka huu. Tangu kujiunga kwa wachezaji hao katika timu hiyo kumeonesha kung’ara. Samata …

Nelson Mandela: Mwana masumbwi hodari

Katika kitabu chake cha “Long Walk to Freedom”, Nelson Mandela hakuficha kueleza mapenzi yake katika mchezo alioupenda na kuucheza – mchezo wa masumbwi.

NUKUU ZA WIKI

Bill Getes: Kukumbuka ulipokosea ni muhimu

Ni vizuri  kusherehekea mafanikio lakini ni muhimu zaidi kukumbuka uliposhindwa awali.

Kauli hiyo ilitolewa na mfanyabiashara mkubwa  wa Marekani na Mwenyekiti wa Microsoft. Bill Gates.

Kwaheri Dk. Mvungi, turejeshe mabalozi wa nyumba 10

Wiki iliyopita ilikuwa ya majonzi makubwa kwangu, na naamini kwa Taifa letu kwa jumla.

Tumempoteza mwanasheria mahiri, Dk. Sengondo Edmund Mvungi, aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba na kucharangwa mapanga. Baada ya Dk. Mvungi kucharangwa mapanga, alipelekwa Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI) na baadaye akakimbizwa nchini Afrika Kusini, alikofia.

Al-Shabaab wapo Tanzania

Matukio ya ugaidi yanayoendelea sehemu mbalimbali hapa nchini, yanathibitisha pasi shaka kuwa kundi la al-Shabaab la nchini Somali tayari lina makazi yake hapa nchini Tanzania.

Oktoba 7, mjini Mtwara walikamatwa vijana 11 wakifanya mafunzo ya ugaidi katika Mlima wa Makolionga wilayani Nanyumbu, na walikutwa wanamiliki silaha za moto, mapanga na DVD 25 zenye miongozo ya mafunzo ya al-Shabaab. Hii ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen.

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (7)

Wiki iliyopita tulichapisha sehemu ya sita katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, ambapo Mwalimu Nyerere anasema wazi kuwa baada ya kushauri ikashindikana, alirejea kijijini Butiama na kuamua kuandika utenzi. Leo, Mwalimu anasimulia nini kilimsukuma kuwaza kuwa uongozi wa CCM ulikuwa umepwaya wa kiwango cha kuhitaji nahodha mpya. “Hawawezi kutetea sera ya Chama ya Serikali Mbili wala mwelekeo wa Chama wa Serikali Moja. Watatumia uwezo walionao kutokana na hadhi walizonazo kuvuruga sera ya Chama na mwelekeo wake. Tutahitaji kiongozi mpya wa Serikali na kiongozi mpya wa Chama.” Endelea…DODOMA 12/11/1993

Nadhani uamuzi wa kuitisha kikao cha mchanganyiko ulifanywa na viongozi wetu katika kikao cha Dodoma II. Nimesema awali kwamba Waziri Mkuu alipohisi kuwa baadhi ya mawaziri wenzake walikuwa wanaunga mkono hoja ya Utanganyika na yeye kwa wakati huo alikuwa hajui aiunge mkono au aipinge, alipendekeza ifanyike semina ya viongozi wote ili jambo hili lizungumzwe na lipingwe nje ya Bunge.