JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: MCHANGANYIKO

Barua ya wazi kwa Rais Kikwete

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, hongera kwa kazi nzuri; siwezi kukupa pole kwani kazi ni kipimo cha utu na wewe unakitekeleza ipasavyo. Mheshimiwa Rais, nakuandikia barua hii kwa masikitiko makubwa baada ya wewe kuwa msikivu…

Tuwe na Serikali mbili zisizonung’unikiana

Hivi sasa Taifa letu liko kwenye mjadala mkubwa wa kijamii na kisiasa katika mchakato muhimu wa kuandika upya Katiba yetu. Mchakato huu umeanza kutokana na kuwapo malalamiko kutoka kwa watu kadhaa kuwa Katiba yetu, ambayo imelilea Taifa letu tangu mwaka 1962, imezeeka, imejaa viraka na hivyo iandikwe upya.

Kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, Desemba 2011 kwamba ataanzisha mchakato wa kuandika upya Katiba yetu, Bunge lilitunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura 83 mwaka 2012 na mchakato ukaanza baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukusanya maoni na kuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba bungeni mapema Machi, 2014.

Bunge Maalum la Katiba sasa linaendelea na vikao vyake Dodoma. Mjadala mkali umezuka na unaendelea kuhusu muundo wa Serikali, baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupendekeza kwenye rasimu ya Katiba kuunda Shirikisho la Serikali Tatu, kinyume cha Katiba ya sasa (Katiba ya mwaka 1977) yenye Serikali Mbili.

Kwanini Zanzibar?

Kwani pale walipotumia chopa tatu kufanya mikutano ya hadhara katika kata 27 kugombea udiwani wananchi si waliwajibu kwa kupata kata tatu tu kati ya hizo 27? Au hivi karibuni walipotumia nguvu yao kubwa katika kuomba Jimbo la Kalenga, hata Chopa ilitumika, mbona wametoka kapa na kiti kikaenda kwa CCM kwa kishindo? Hivyo vyote si vinaashiria kutokubalika kwao? Kwanini hawasomi ishara za nyakari na wakatambua mbinu hiyo ya mikutano ya hadhara na wananchi haina tija?

Kumbe ndio maana Lukuvi anashambuliwa

Msimamo wa kutaka kila kitu kifanyike bila ubabaishaji katika kamati na wizara zinazomhusu, umetajwa kuwa ndio unaomgharimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Miongoni mwa nyadhifa kubwa alizo nazo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni pamoja na ujumbe wa Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Bodi ya Wakurugenzi TPA haina meno mbele ya Kipande

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) haina meno mbele ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hiyo, Madeni Kipande, baada ya kubainika kuwa maelekezo mengi anayopewa na Bodi anayapuuza.

Baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuunda Kamati ya Mbakileki kuchunguza kinachoendelea bandarini wakati wa uongozi wa Ephraem Mgawe, Kamati ilitoa mapendekezo ambayo bodi ilimwagiza Kipande kuyatekeleza, lakini zaidi ya asilimia 90 ya mapendekezo hayo ameyapuuza.

Nyalandu apangua ‘amri’ ya Nyerere

*Aagiza wataalamu wafungue mpaka wa Bologonja

*Watalii kutoka Kenya wataingia kiulaini Serengeti

*Watafaidi vivutio, kisha fedha zote zitaishia Kenya

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameshakamilisha mipango ya kufungua mpaka wa Bologonja; jambo linalotajwa kuwa ni pigo kwa uchumi wa Taifa na kwa wadau wa tasnia ya utalii nchini.

Mpaka huo unaotenganisha Tanzania na Kenya, ulifungwa mwaka 1977 kwa amri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi na kimazingira ya Taifa.

Taarifa zilizopatikana kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii zinasema tayari Nyalandu ameshawaagiza viongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na wengine katika Wizara yake, kuhakikisha mpaka huo unafunguliwa.

Mkurugenzi  Mtendaji wa TTB, Aloyce Nzuki, ambaye Nyalandu amemwondoa kwenye nafasi hiyo, anatajwa kuwa mmoja wa watu waliopinga mpango huo kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake. Upinzani huo unatajwa kuwa miongoni mwa sababu alizotumia Nyalandu kushinikiza Nzuki aondolewe.