JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Magazetini

Sababu ya kutokukubalika ushahidi wa kuambiwa 

Na Bashir Yakub Ushahidi wa kuambiwa ni ushahidi unaotolewa na mtu ambaye hakuona tukio likitendeka, hakusikia tukio likitendeka, hakuhisi wala kuonja, wala kunusa hilo, bali aliambiwa na mtu mwingine aliyeona, kusikia, kuhisi, kunusa au kuonja.  Zifuatazo ni sababu kwanini ushahidi huu haukubaliki:- (A)  Sheria ya Ushahidi Kifungu cha 61 na 62 kinauweka ushahidi wa kuambiwa katika ushahidi wa maneno (oral evidence). Na kanuni za ushahidi wa maneno ni kuwa ili uweze kukubalika kama ushahidi sahihi ni lazima kama swali ni nani aliyeona tukio likitendeka, basi  jibu awe nalo mtu aliyeona tukio likitendeka, na kama swali ni nani aliyesikia tukio likitendeka, jibu awe nalo aliyesikia tukio likitendeka, na kama swali ni nani aliyehisi au kuonja kitu fulani, jibu awe nalo mwenyewe kabisa aliyehisi au kuonja kitu hicho, na kama swali ni mtaalamu yupi alipima na kugundua kuwa jambo fulani lilisababishwa na kadha wa kadha, jibu awe nalo mtaalamu huyohuyo na si vinginevyo.  Hii ndiyo kanuni inayoongoza ushahidi wote wa maneno…

Vijana tusiishi na faraja

Vijana ni nguvu kazi ya taifa. Wao ndio tegemeo kubwa la kujenga na kuleta maendeleo ya taifa, hasa katika taifa linalokusudia kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na kijamii. Ni yumkini taifa lisilo na vijana ni ufu. Vijana hawa wapo wa…

Katiba imara bila taasisi imara ni unyang’au tu!

DODOMA Na Javius Byarushengo Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, alipofanya ziara nchini Ghana mwaka 2009 akiwa madarakani, alisema kuwa ili Bara la Afrika lipate maendeleo, halihitaji kuwa na watu imara bali taasisi imara. Kimsingi Obama, Mmarekani wa kwanza…

UHURU WA MAREKANI:  Je, inajifunza kutokana nao?

Zanzibar Na Masoud Msellem Julai 4, kila mwaka dola ya Marekani huadhimisha siku ya kumbukumbu ya uhuru wake. Mwaka huu inaadhimisha uhuru huo ikiwa ni miaka 245 tangu iupate kutoka kwa Himaya ya Uingereza mwaka 1776.  Uhuru huo ulipatikana baada…

Agizo la Waziri TAMISEMI latekelezwa

GEITA Na Antony Sollo  Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita limetekeleza agizo lililotolewa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde, kwa kuwaweka kando kupisha uchunguzi watumishi watatu wa…

Diwani alilia magofu ya Serikali

DAR ES SALAAM Na Alex Kazenga Pamoja na serikali kutilia mkazo ujenzi wa sekondari na vituo vya afya kila kata, Kata ya Minazi Mirefu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam hali ni tofauti. Kata hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 yenye wakazi…