Category: Kimataifa
79 wafariki baada ya paa kuporomoka klabuni Jamhuri ya Dominika
Watu 79 wamekufa baada ya paa la klabu moja maarufu ya usiku katika Jamhuri ya Dominika kuporomoka. Miongoni mwa waliokufa katika tukio hilo la usiku wa manane ni mwanasiasa mmoja na mchezaji nyota wa Baseball. Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa…
Walionyongwa duniani waongezeka : Amnesty
Idadi ya watu wanaojulikana kunyongwa mwaka jana ilikuwa kubwa zaidi katika takriban muongo mmoja, huku Iran, Iraq na Saudi Arabia zikiongoza kwenye orodha ya nchi zilizotekeleza hukumu hiyo. Ripoti ya kila mwaka kuhusu ya hukumu za kifo ya Shirika la…
Kagame azilaani nchi zinazoiwekea Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame amezilaani nchi zinazoiwekea nchi yake vikwazo. Baadhi ya mataifa yameiwekea Kigali vikwazo kuhusu kuhusika kwake katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Akihutubia kwenye tukio la kuashiria mwanzo wa mfululizo wa shughuli…
Ukraine na Marekani hatimaye kusaini mkataba wa madini
Timu ya wapatanishi wa Ukraine itasafiri kwenda Marekani wiki hii, wakitarajia kusaini mkataba wa madini ambao umekwama kwa wiki kadhaa. Washington pia inataka haki za kuchimba madini nchini Ukraine kwa kubadilishana na misaada inayoipa nchi hiyo. Mkataba huo ulitarajiwa kutiwa…
Trump atangaza mazungumzo ya nyuklia na Iran
Rais Donald Trump amesema Marekani itaanzisha mazungumzo, ya ngazi ya juu na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia siku ya Jumamosi. Alitoa tangazo hilo la kushangaza alipokutana na Netanyahu katika Ikulu ya White House. Rais huyo wa Marekani alisema ana…
Israel yaendeleza mashambulizi Ukanda wa Gaza
Mashambulio ya Israel yasababisha mauaji ya watu wawili akiwemo muandishi habari na kuwajeruhi wengine tisa, Ukanda wa Gaza. Israel imeshambulia mahema yanayotumiwa kama makaazi na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ,nje ya hospitali mbili kubwa kwenye Ukanda huo na kuua…