Category: Kimataifa
Hezbolllah yasema ilirusha makombora zaidi ya 320
Kundi la Hezbollah limesema kwamba limerusha makombora zaidi ya 320 kuelekea Israel alfajiri ya Jumapili. Katika taarifa iliyotolewa mapema Asubuhi, kundi hilo lilisema kwamba lililenga maeneo kumi na moja ya kijeshi kaskazini mwa Israel kwa kutumia maroketi za aina ya…
Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora na droni
Ukraine imesema Urusi imevurumisha makombora na droni kwa usiku kucha ikilenga maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Ukraine. Aidha Jeshi la Anga Ukraine limeongeza kwamba droni nane kati ya tisa zilizorushwa na Urusi ziliharibiwa na mifumo ya anga ya Ukraine…
Dola milioni 18.5 kudhibiti Mpox
Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji (IOM), limeomba msaada wa dola milioni 18.5 kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watu walioathiriwa na mripuko wa homa ya Mpox Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkurugenzi Mkuu wa IOM,…
WHO: Mpox sio aina mpya ya UVIKO
Shirika la Afya Duniani WHO limetoa tamko rasmi leo Jumanne la kusisitiza kwamba ugonjwa wa homa ya nyani unaosababishwa na virusi vya mpox, sio ugonjwa mpya wa UVIKO unaosababishwa na virusi vya corona. Tamko hilo limetolewa baada ya kuibuka kwa…
Serikali ya Ruto kurejesha vipengee vya mswada wa fedha
Serikali ya Kenya imesema italazimika kurejesha baadhi ya hatua za ulipaji kodi ambazo zilifutwa baada ya kuibuka maandamano makubwa mwezi Juni. Hatua ya Serikali ya Kenya ni jambo linalozidisha hatari ya kutokea machafuko zaidi katika taifa hilo la Afrika Mashariki….
Zelensky: Wanajeshi wetu wanatimiza malengo yao huko Kursk
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wanatimiza malengo yao kufuatia mashambulizi katika eneo la Urusi la Kursk, yaliyoanzishwa karibu wiki mbili zilizopita. Kwenye hotuba yake, Zelensky amesema “nimepokea ripoti kutoka kwa Kamanda Mkuu wa jeshi Syrskyi kuhusu hali…