Category: Habari Mpya
JPM ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KENYATTA
Rais Dkt Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia ajali kati ya basi la abiria na lori la mizigo, iliyopelekea vifo vya watu takribani 36 na wengine kujeruhiwa iliyotokea jana asubuhi.
PPF WAMKANA MFANYAKAZI WAO ALIYEKAMATWA NA MIRUNGI
MFUKO wa Pensheni wa PPF umesema mfanyakazi wake, Anitha Oswald, wa ofisi ndogo ya Moshi aliyekamatwa wiki hii akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi huko Moshi, Kilimanjaro, alikuwa kwenye likizo ya dharura na kwamba alikamatwa akiwa kwenye gari…
MTANGAZAJI WA UHURU FM, LIMONGA JUSTINE LIMONGA AFARIKI DUNIA
Tanzia: Mtangazaji wa kipindi cha Michezo cha Uhuru FM Justin Limonga amefariki Dunia Leo asubuhi katika hospital ya TMJ alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. R.I.P Mpendwa wetu Limonga
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU LA DAR ES SALAAM LATOA TATHMINI YA MATUKIO YA UHALIFU MWAKA 2017
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, Lazaro Mambosasa, leo Desemba 29, 2017 limetoa ripoti yake ya matukio ya kihalifu na oparesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo kwa mwaka 2017. Akizungumza na waandishi wa…
MAHAKAMA YA KISUTU YAAGIZA UPELELEZI KUKAMILIKA HARAKA KESI YA DR TENGA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk.Ringo Tenga. Mbali na Dk. Tenga, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na…
TANZIA: MWANDISHI IDD SALUM MAMBI AMEFARIKI DUNIA
Aliyekuwa mpiga picha wa kituo cha runinga cha Azam, Iddi Mambo amefariki dunia baada ya kuugua ghafla. Msiba upo nyumbani kwao Kawe Ukwamani. “Innalillahi Wa Inna Ilaihi Rajiun”