Category: Habari Mpya
Magufuli achukua mkondo mpya
Ugumu wa upatikanaji wa fedha ulioibua msemo maarufu wa “vyuma vimekeza”, umebadilika kwa serikali kuanza ‘kulegeza’ baadhi ya mambo. Manung’uniko yameanza kupungua mitaani ambako fedha ziliadimika kwa kiwango kikubwa kuanzia mwaka 2016, lakini Rais John Magufuli akisema waliokuwa wakilalamika ni…
TAZARA ‘imeuzwa’
Mkakati maalumu wa kuiua Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) unaohusisha kukodisha reli kwa shirika binafsi umefichuliwa, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini. Pamoja na kukodisha reli, kiwanda cha kuchakata kokoto cha Kongolo, mali ya mamlaka hiyo kinatafutiwa ‘mnunuzi’….
Lissu njia panda
Ofisi ya Bunge inakusudia kutangaza hatima ya ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), baada ya kutokuwapo bungeni kwa miezi 16 sasa. Uamuzi huo ukisubiriwa kutoka kwa Spika Job Ndugai, mwanasiasa huyo amekataa kuzungumzia lolote kuhusu madai kwamba…
Spika, CAG ngoma nzito
Kama ungekuwa mchezo wa soka, basi ungesema zimechezwa dakika 90 zimekwisha, zikaongezwa dakika 30 zikaisha timu zikiwa sare, sasa wanaelekea kwenye kupiga penalti. Huo ndiyo mchuano uliopo kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa…
Siri zavuja Jiji
Siri nzito za mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha mabasi ya kwenda mikoani eneo la Mbezi Luis zimevuja, zikavuruga watendaji na Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, JAMHURI linathibitisha. Baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuandika…
Benki yaibia wateja
Maofisa wa Bank of Africa (BOA) jijini Dar es Salaam wanadaiwa kughushi hati ya ardhi Na. 55709, Kitalu ‘C’, Ukonga Stakishari ya Jimmy Mwalugelo (68), mkazi wa eneo hilo na kuitumia kumkopesha mtu mwingine Sh milioni 500. Hati hiyo iliyoghushiwa…