JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Habari Mpya

Ndejembi awakumbusha wanafunzi UDOM kuzingatia maadili

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuishi kwa kuzingatia maadili ya kitanzania ili kutimiza malengo yao kitaaluma na kujenga taswira nzuri ya chuo…

Serikali yatoa bil.7/- kutekeleza mradi wa maji Ludewa

Serikali imetoa zaidi ya Sh.bilioni 7 kwa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA),kwa ajili ya kutekeleza mradi  mkubwa wa maji katika mji wa Ludewa mkoani Njombe. Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo alisema hayo jana, wakati akizungumza na baadhi ya wananchi na viongozi wa wilaya ya Ludewa akiwa katika ziara yake ya kukagua na kutembelea miradi ya maji mkoani Njombe. Alisema,kwa sasa Serikali kupitia Ruwasa iko katika  mchakato wa kumpata mkandarasi atakayeweza kutekeleza mradi huo unatarajiwa kumaliza kabisa tatizo la maji kwa wananchi wa Mji wa Ludewa na vijiji vya jirani kwa asilimia mia moja. Amewaagiza viongozi wa RUWASA wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe,kuhakikisha wanatafuta mkandarasi mwenye uwezo mkubwa wa kifedha ambaye atatekeleza kazi  kwa wakati na bila usumbufu wowote. “Kwanza naagiza wataalam wangu wamtafute mkandarasi mwenye nguvu ya kifedha  ambaye akianza kutekeleza kazi ya Sh. milioni hamsini kati ya bilioni 7 asisimame,tunamtaka mkandarasi ambaye hata fedha zikichelewa aendelee na kazi ili wananchi wafaidi matunda ya serikali yao”alisema Kivegalo. Aidha,amewataka wataalam wa Ruwasa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya maji wakiwamo wataalam wa mabonde ya maji,kuhakikisha wanadhibiti na kutunza vyanzo vyote vya maji ili mradi huo uliosanifiwa kufanya kazi kwa miaka ishirini ijayo uwe endelevu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kivegalo ameishukuru Serikali kutoa fedha hizo na kuhaidi kuwa,zitafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kuwahakikishia wananchi wa Ludewa kuwa, huduma ya maji  katika mji huo itakuwa safi na salama. Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ludewa Enock Ngoyinde alisema,mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Sh.bilioni 7.4 na utahudumia zaidi ya wakazi 15,661 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia ishirini na tatu. Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamoga,ameipongeza serikali ya awamu ya sita  kuendelea kuipatia wilaya ya Ludewa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika vijiji mbalimbali vya jimbo la Ludewa. Alisema, katika kipindi kifupi serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa), imefanikiwa  kutekeleza miradi ambayo imewezesha kupunguza kama sio kumaliza kabisa changamoto ya maji safi na salama kwa wakazi wa jimbo hilo. Hata hivyo,ameiomba wizara ya maji kujenga miradi  mingine katika vijiji vilivyopo kando kando ya Mto Ruhuhu ili kuwanusuru wananchi na hatari ya kuliwa na wanyama wakali hasa mamba na kutumia maji ya mto huo ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

NIT yapokea ithibati za mafunzo ya kozi ya uendeshaji ndege

Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimepokea ithibati mbili za mafunzo ya kozi ya usafiri wa anga yaani kozi ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege na uendeshaji wa safari za ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga…

Majaliwa: Tutumie mapato ya ndani kutekeleza miradi

………………………………………………………………………………………………………………………………….. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri nchini kutumia fedha za makusanyo ya ndani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo badala ya kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu pekee. Amesema hayo leo (Jumapili, Novemba 27, 2022) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi…

Serikali yaombwa kupiga tafu ujenzi wa kituo cha afya Liwale

Serikali imeombwa kukiunga Mkono Kijiji Cha Nambinda kilichopo katika Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi katika kufanikisha utekeleza wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo Ujenzi wa kituo Cha Afya. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nambinda Said Abdala Kowe wakati…