JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Sitanii

Prof. Lipumba aseme ukweli wote

Leo bado siku 75 kabla ya Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25. Muda unaweza kuonekana mwingi, lakini ni mchache. Matukio yanayoendelea katika ulingo wa siasa, uvumi na taarifa zinazosafiri kama moto wa nyasi kavu, yanatupasa kuwa makini na kuchambua pumba…

Lowassa si sawa na Mrema

Hiki ni kipindi cha Uchaguzi Mkuu. Oktoba 25, wananchi watakwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Wananchi watakuwa na jukumu la kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wake (mgombea mwenza). Kwa Wazanzibari, mbali na Rais na Makamu…

Mauaji ya koromeo tishio Kagera

Kwa muda wa mwezi mmoja sasa nipo hapa mkoani Kagera. Nazunguka katika wilaya mbalimbali kuangalia maendeleo ya Mkoa wa Kagera.  Nimepata fursa ya kufika Kayanga Karagwe, nimeishia kupata mshangao. Nimeshangaa kwani Kayanga niliyoiacha ikiwa na majengo mawili mwaka 2001; Tindamanyile…

Sasa naliona anguko la CCM

Miezi miwili iliyopita niliandika makala katika safu hii yenye kichwa cha habari kisemacho: “CCM inaanguka taratibu kama dola ya Warumi”. Katika makala hiyo, nilieleza kuwa viongozi wapo kwenye sherehe na safari za ugaibuni. Kwa nadra sana wanafahamu kinachoendelea nyumbani. Dola…

CCM iruhusu ushindani wa haki urais

Kwa wiki takribani nne hivi, sijaonekana katika safu hii. Sikuonekana kutokana na matatizo ya msiba, lakini pia nikalazimika kufanya kazi mikoani. Huku niliko nakumbana na tunachopaswa kupambana kukiondosha. Sehemu nyingi za mikoani hakuna huduma ya data (Internet), simu zipo ila…

Bandari Bagamoyo, kifo cha Bandari Dar

Imenichukua miaka miwili kufikiri juu ya hiki kinachoitwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Ujenzi huu ulianza kutajwa mwaka 2010, na ilipofika Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, akatia saini mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo. Mkataba ukasema bayana kuwa…