JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Sitanii

Nakubaliana na Marando, Tanzania ina bahati

Miaka mitatu iliyopita Mwanasheria maarufu nchini, Mabere Marando alitoa kauli ambayo si mimi tu, bali Watanzania wengi hatukumwelewa. Kauli yenyewe ilikuwa hivi: “Tanzania ni nchi yenye bahati. Ni nchi pekee duniani inayojiendesha bila Rais.” Wapo walioichukulia kama vijembe vya kisiasa,…

Rais Magufuli epuka mitego ya Kikwete (2)

Leo naandika sehemu ya pili ya makala hii. Naomba niseme kuwa nimefarijika kutokana na mrejesho mkubwa kutoka kwenu wasomaji wangu. Nimefarijika kuona makala hii inanikutanisha na marafiki tuliopotezana miaka 30 iliyopita. Yupo mmoja wa marafiki zangu mara ya mwisho tumekutana…

Rais Magufuli epuka mitego ya Kikwete

Wiki mbili zilizopita sikuandika katika safu hii. Sikuandika kwa maana kwamba nilikuwa mbio nasafiri mkoa hadi mwingine, kwa kiwango kilichonifanya nishindwe kutimiza wajibu wangu. Lakini si hilo tu, matokeo kadri yalivyokuwa yanatoka, taarifa zinasambaa ilinilazimu kufunga breki kwanza, kwa nia…

Kwaheri Deo, Lowassa kukamilisha historia!

Usiku wa Alhamisi ya Oktoba 15, nikiwa jijini Mwanza nilipata taarifa za ajali ya helikopta. Taarifa hizi mwanzo zilitaja viongozi wanne waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa walikuwamo. Moyo wangu ulikwenda mbio. Nilimtafuta mmoja wa viongozi wa juu wa…

NEC haina mamlaka kumtangaza aliyeshindwa

Leo (Jumamosi Oktoba 10) naandika makala hii ikiwa zimesalia siku 15 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika. Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 25, siku ya Jumapili. Kanisa Katoliki tayari limetangaza kuwa ibada ya Jumapili kwa baadhi ya majimbo itafanyika Jumamosi ya Oktoba…

Sasa ni Lowassa, Magufuli

Leo naandika makala hii nikiwa mkoani Tanga. Naandika makala hii zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25. Nimepata fursa ya kusafiri maeneo mbalimbali ya nchi hii. Nimezungumza na watu mbalimbali. Nimesikiliza ahadi za wagombea urais Edward Lowassa…