Na Wilson Malima JAMHURI MEDIA, Dodoma.

Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amepewa zawadi ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe.

Rais Samia amepokea zawadi hiyo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo wa Dkt. Patrice Motsepe aliyekuwa ameambatana na Rais wa Shririkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Dkt. Wallace Karia pamoja na viongozi wengine katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma leo Oktoba 20, 2023.

Kwa Mujibu wa tovuti ya www.yourdictionary.com Pennant ni zawadi ambayo hutolewa kwa timu fulani baada ya kutwaa ubingwa au kwa mtu aliyechagiza kuleta ubingwa wa mashindano ya ligi katika mchezo wa soka au ‘baseball’.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika zawadi yake ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kama kumbukumbu mara baada ya kupewa na Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kama kumbukumbu kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro watatu kutoka (kulia), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma wa pili kutoka kulia, Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria Mhe. Jaji George Masaju wa kwanza (kulia), Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wa pili kutoka kushoto pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Neema Msitha wa kwanza (kushoto) mara baada ya mazungumzo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Oktoba, 2023.