Skip to main content
JAMHURI MEDIA
Tunaanzia wanapoishia wengine
Home
Kitaifa
Biashara
Siasa
Uchumi
Kimataifa
Makala
Siasa
Uchumi
MCHANGANYIKO
Michezo
Burudani
Kazi/Ajira
Gazeti La Jamhuri
Sitanii
JAMHURI YA WAUNGWANA
Nyundo ya Wiki
Search
November 7, 2022
Habari Mpya
Bunge la Afrika laombeleza vifo vya watu 19 ajali ya ndege
Jamhuri
Comments Off
on Bunge la Afrika laombeleza vifo vya watu 19 ajali ya ndege
Wabunge wa Bunge la Afrika (PAP) wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka Watanzania waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyotokea nchini Tanzania Jumapili Novemba 6,2022 katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Picha na Kadama Malunde – Midrand Afrika Kusini
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira akiongoza Mkutano wa Bunge la Afrika leo Jumatatu Novemba 7,2022
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kushoto) akimpa pole Mbunge wa Bunge la Afrika kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anatropia Theonest kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kufuatia ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyoua watu 19 baada ya kuanguka katika Ziwa Victoria Nchini Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wote wametuma salamu zao za faraja kwa familia za waathirika wa ajali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila ametaja marehemu kuwa ni pamoja na Neema Faraja, Hanifa Hamza, Aneth Kaaya, Victoria Laurean, Said Malat Lyangana, Iman Paul, Faraji Yusuph, na Lin Zhang.
Wengine ni Sauli Epimark, Zacharia Mlacha, Eunice Ndirangu, Mtani Njegere, Zaituni Shillah, Dk Alice Simwinga na afisa wa kwanza wa ndege hiyo, Peter Odhiambo.
Hakuna miili mingine iliyopatikana. Taarifa za awali zilieleza kuwa ajali hiyo ilitokana na hali mbaya ya hewa. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha shughuli zote za ndege katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa muda usiojulikana.
Shirika la ndege la AirTanzania, pia limesitisha safari zake Jumapili kuelekea Bukoba.
Timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa sasa ipo mjini Bukoba kuchunguza tukio hilo
Post Views:
286
Previous Post
Ugonjwa wa figo unavyogharimu maisha
Next Post
Kijana aliyeokoa watu ajali ya ndege Serikali 'yamuheshimisha'
Msafara wa kiongozi ACT Wazalendo Dorothy akiwasili Lindi kufunga kampeni
Waziri Kabudi azindua siku 16 za uarakati za kupinga ukatili Dar es Salaam
Mamia wajitokeza huduma za uchunguzi wa macho Hospitali ya Mbagala
Kumkamata Netanyau haitoshi lazima apate adhabu ya kifo – Iran
Kesi ya Donald Trump yatupiliwa mbali na jaji wa mahakama
Habari mpya
Msafara wa kiongozi ACT Wazalendo Dorothy akiwasili Lindi kufunga kampeni
Waziri Kabudi azindua siku 16 za uarakati za kupinga ukatili Dar es Salaam
Mamia wajitokeza huduma za uchunguzi wa macho Hospitali ya Mbagala
Kumkamata Netanyau haitoshi lazima apate adhabu ya kifo – Iran
Kesi ya Donald Trump yatupiliwa mbali na jaji wa mahakama
Soma Gazeti la Jamhuri Novemba 26 hadi Desemba 2, 2024
Tanzania kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kukuza utalii
Polisi yawasaka waliomshambulia mtoto na kumjeruhi Monduli
Waandishi wa habari Manyara, UTPC waandamana uzinduzi Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili
Vyama vya siasa, wananchi wahimizwa amani uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
JWT: Wafanyabiashara bado tuna changamoto nyingi
Kilo 2207 za dawa za kulevya zanaswa
RC Ruvuma : Hali ya maambukizi ugonjwa wa UKIMWI yapungua, ashauri kuendelea kujikinga
Mkakati: CCM ikihitimisha kampeni kwa kishindo
TPA bingwa mashindano ya SHIMMUTA 2024