Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ambaye atakumbukwa kwa kufuta uchaguzi 2025 na kupata umaarufu, Jecha Salim Jecha amefariki dunia katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Marehemu akiwa Mwenyekiti wa Tume hiyo aliwahi kufuta matokeo ya uchaguzi kisiwani Zanzibar akidai uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria.
Maziko yanatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar. Inna Lillah Waina Ilaihi Rajuum