Baraza la Mitihani (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa wanne wa kidato cha nne mwaka 2022 walioandika lugha za matusi kwenye mitihani yao.
Hayo yamesemwa leo Januari 29,2023 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne yaliyofanyika mwaka jana 2022,amesema kati ya watahiniwa hao mmoja ni wa maarifa (QT) na 332 watahiniwa wa shule.
NECTA pia limewafutia matokeo yote watahiniwa 333 moja wa QT na 332 wa mtihani wa kidato cha nne ambao wamebainika kuwa wamefanya udanganyifu kwenye mitihani yao.
Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha No.5(2) (1 na J) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107 kikisomwa pamoja na kifungu chan 30 ()2) (b) cha kanununi za mitihani 2016.