Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Vigwaza
WATU wanne kati yao wakiwa ni wanawake watatu na mtoto mmoja wamefariki dunia agost 22,2024 saa 8 mchana katika ajali iliyotokea barabara Kuu ya Morogoro eneo la Vigwaza mkoani Pwani.
Aidha wapo majeruhi kadhaa ambao idadi bado haijafahamika.
Ajali hiyo imehusisha basi la abiria iliyokuwa ikitokea Dodoma yenye namba za usajili T277 DCN kampuni ya Baraka na lori la mafuta linalotokea nchini Rwanda ,lenye namba RL 3520 .
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo akitoa taarifa za awali za ajali hiyo alieleza ,dereva wa basi la kampuni ya Baraka alikuwa akijaribu kupita magari mengine bila tahadhari aligongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo hivyo.
Alieleza, waliofariki ni watano ikiwa ni wanawake wattatu na mtoto mmoja ambapo majina yao hayajapatikana na majina ya majeruhi.
“Hadi sasa tunaendelea na uchunguzi na taarifa zaidi za majina ya marehemu na majeruhi tutatoa baadae”
Lutumo alifafanua, majeruhi wapo kituo cha afya Mlandizi kwa matibabu.
Lutumo pia alieleza kwamba, marehemu wamehifadhiwa katika kituo cha afya Chalinze na watatoa taarifa zaidi.
Alitoa wito kwa madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani na kueleza uzembe unasababisha vifo , majeruhi wasio na hatia ,msongamano wa magari ajali zikitokea na kusababisha hasara .