Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia
Dar es Salaam

BONDIA wa ngumi maarufu nchini Karim Mandonga amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kuunga mkono mchezo wa ngumi na kuanza akitoa zawadi kwa washindi wa mapambano mbalimbali ili kuwapatia hamasa.

Mandonga ametoa shukrani hizo mapema jioni Desemba 31, 2024 ikiwa imebaikia masaa kadhaa kuelekea sherehe za mwaka mpya 2025 akizungumza na waandishi wa habari Makunduchi Villa Hotel, Ungindoni, Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Amesema lengo la kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa “kusapoti” mchezo wa ngumi nchini ambapo yeye ni miongoni mwa mabondia ambao tayari wameshafikiwa na zawadi yake baada tu ya kumaliza shindano lake Mkoani Kagera.

“Hakuna mwingine kama Mama “Rasi Samia”,nimeamini uvumilivu ni jambo pekee sana katika maisha ya mwanadamu na muda ukifika hakuna wa kuzuia nimekuja kumshukuru kwa namna anavyotusapoti Mabondia, tumeaona amekuwa akisapoti mchezo wa mpira wa miguu, kuwamekuwa na goli la Mama, sasa ni zamu yetu na sisi wa mchezo wa ngumi kupata zawadi yake,” alisema Mandonga.

Mandonga alisema kuwa “sapoti” hiyo ya Rais Dkt. Samia inawapa hamasa mabondia wapambane na kushinda mapambano yao kwasababu watapata zawadi za mapromota pamoja na ya Rais Samia hivyo maisha yao yatakuwa mazuri

Mandonga alieleza kwamba kwa makubwa anayofanya Rais Samia katika Sekta mbalimbali nchini ikiwemo hiyo ya michezo, Afya, elimu, miundombinu na nyingine, anafaa kuungwa mkono ili aendelee kufanya mazuri zaidi.

Aidha Mandonga ameahidi kujitolea kutangaza mazuri ya Rais Samia ili wananchi wayajue na hatimaye apewe mitano tena ya Uongozi katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Hata hivyo Mandonga alisema atampelekea zawadi ya mkanda wake wa PST alioupata katika pambano lake Ikulu

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makunduchi Villa Hotel Mohammed Haji alisema amekuwa akimuunga mkono Mandonga kwa sababu amekuwa akiunga mkono mambo mabalimbali yanayofanywa na Rais Samia hivyo vijana wengine waamuke kuchangamkia mchezo huo

Hivyo kwa sababu alikuwa na jambo la kuzungumza kuhusu Rais Samia akamsapoti kwa kumtengenezea mazingira ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kufikisha ujumbe wake.

Hata hivyo Haji alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono michezo ikiwemo mchezo huo wa ngumi.

Mkurugenzi amebainisha kuwa kuelekea mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika kwa uenyeji wa Tanzania, wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye ujenzi wa mahoteli kwani Kutakuwa na ugeni mkubwa watahitaji sehemu za kupata malazi hivyo ni.fursa pekee ya kuhakikisha wanaifurahia Tanzania na wakiondoka wakaitangaze vizuri nchini kwao.