Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu wa Iran ukiongozwa na Balozi wake nchini Tanzania, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh tarehe 27 Oktoba, 2023 jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mambo mengine, nchi ya Iran imeonyesha nia ya kufanya uwekezaji na biashara katika Sekta ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania.