Rais wa Marekani Joe Biden ameghadhabishwa na hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhali wa Jinai, ICC- iliyotoa hati ya kumkamata Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kuhusiana na mashtaka ya uhalifu wa kvita huko Gaza.
Marekani si mwanachama lakini kunaonekana kuwa na mgawanyiko hata miongoni mwa wanachama.
Serikali ya Uingereza haijatoa tamko lolote. Hata hivyo mbunge mmoja wa chama tawala cha Leba Emily Thornberry anasema nchi yake inawajibu wa kutekeleza amri ya mahakama hiyo ya ICC ikihitajika kufanya hivyo iwapo Netanyahu atathubutu kuingia Uingereza.
“Tuliweka saini kuridhia mkataba wa Roma unaotoa taratibu za utendaji kazi wa mahakama hiyo -kwa hivyo majukumu yetu kuhusu hilo yako wazi …kwa kifupi, tuwaunga mkono mahakama hiyo ya kimataifa ICC.Ni koti huru na kama imeamua Netanyahu ana kesi ya kujibu mbele yao, na tayari wametoa waranti kwamba akamatwe, basi hatuna budu kuzingatia hatua hiyo, alisema.