Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya NMB Wilaya ya Kigamboni. Wengine ni viongozi waandamizi wa Benki hiyo na Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Bw. Hashim Mgandilwa (kushoto) pamoja na Mkurungezi Mtendaji
wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Tawi
jipya la Benki ya NMB Wilaya ya Kigamboni.
BENKI ya NMB imezindua tawi jipya eneo la Kigamboni jijini Dar, ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za kibenki kwa wateja na Wananchi kwa ujumla.
Tawi hilo la kwanza kwa taasisi za fedha kuzinduliwa wilaya ya Kigamboni, limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ms. Ineke Bussemaker alisema huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB katika kusogeza huduma kwa wateja wake.
Alisema tawi hilo jipya la Kigamboni litarahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wateja wake hali ambayo itapunguza mzunguko wa wananchi kuzifuata huduma za kibenki.
Aliongeza kuwa NMB imezingatia shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa Kigamboni kwa wafanyabiashara, wavuvi, wakulima, utalii wa ndani na kufungua tawi hilo hivyo wateja hawatalazimika kuvuka maji kwenda mjini kupata huduma za kibenki kama zamani.
Bi. Bussemaker aliongeza kuwa kwa kutumia Fanikiwa Account, wafanyabiashara wanaweza kunufaika na mikopo inayotolewa kuanzia shs 500,000 na kuendelea kukuza biashara zao. NMB tunakuwa pamoja na biashara yako kupitia Akaunti ya Fanikiwa.
Alisema NMB sio kwamba tu ni benki kubwa nchini, bali inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kijamii kwani inatenga takribani shilingi bilioni moja kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika jamii hasa kuinua elimu na afya.
“Huduma hii ya kibenki kutumia simu za wateja zinamwezesha mteja wetu kupata huduma saa 24 na siku saba za wiki kwa uhuru zaidi…tunawashauri wateja wetu kutembelea ATM zetu au matawi kwa ajili ya kujiunga na huduma ya NMB Mobile na kufurahia huduma hiyo kupitia namba *150*66#,” alisema.
Kwa kuona umuhimu wa kusongeza huduma kwa wateja hasa maeneo ya vijijini Benki ya NMB inaendelea kuwawezesha mawakala watakaosaidia kutoa huduma hizo jambo ambalo litasaidia kusogeza hudumakwa wateja wetu.
Aliongeza, kwa sasa Benki hiyo ina matawi 218 na zaidi ya mashine za kutolea fedha (ATM) 800 nchi nzima pamoja na vituo vya mawakala 947 wa jijini Dar es Salaam, kwa kufungua tawi hili NMB inakuwa benki ya kwanza kufungua tawi Kigamboni.
Benki ya NMB imekuwa ikitoa kipaumbele katika utoaji huduma kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kurahisisha huduma kwa wateja wake pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za wateja hadi sasa NMB ina zaidi ya wateja milioni1.5 wanaonufaika na huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi.