Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ukiwa katika kikao na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, wakiwa katika kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini humo.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, akizungumza wakati wa kikao na Ujumbe wa Tanzania ambao uliongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini humo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao cha Ujumbe wa Tanzania ambao uliongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini humo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango – Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, akizungumza wakati wa kikao cha Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini humo.
…………………..
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuidhinishia Tanzania miradi 14 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.87, kupitia mpango wa Benki hiyo wa utoaji mikopo na misaada (IDA-20), zilizoelekezwa katika miradi ya sekta za elimu, afya, hifadhi ya mazingira, miundombinu, nishati na Tanzania ya Kidigiti.
Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, wakati wa Mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), jijini Washington DC, Marekani.
Alisema kuwa miradi hiyo 14 ni kati ya miradi 25 ya kimkakati yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5, ambayo Serikali iliiwasilisha kwenye Benki hiyo kwa ajili ya kupatiwa fedha ili iweze kutekelezwa na kuchangia kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi, maendeleo ya nchi na kupunguza umasikini kupitia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya 2025.
Dkt. Nchemba aliishukuru pia Benki hiyo kwa kutoa Awamu ya Kwanza ya kiasi cha dola za Marekani milioni 500 kati ya kiasi cha dola milioni 750, mwezi Desemba mwaka 2023, kwa ajili ya kuchangia Bajeti ya Serikali, ili kukabiliana na athari za Uviko-19 na vita vinavyoendelea baina ya Ukraine na Urusi kwa kuwekeza kwenye miradi inayochochea uchumi na huduma za jamii.
Aidha, Dkt. Nchemba aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuahidi kusaidia ujenzi wa mradi wa Kikanda wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mradi ambao ni muhimu kwa ajili ya kuchochea biashara, ukuaji wa uchumi, kuboresha mtandao wa miundombinu ya usafiri na usarishaji, kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na kukuza ajira katika ukanda huo.
Akizungumza katika Mkutano huo, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayezisimamia nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, aliipongeza Tanzania kwa hatua mbalimbali inazozichukua katika kusimamia uchumi na maendeleo ya wananchi wake na kwamba mafanikio hayo yanapaswa kuigwa na nchi nyingine.
Aliahidi kuwa Benki ya Dunia iko tayari kuendelea kuisadia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake ya maendeleo kwa kuipatia fedha na utaalam kwa kuziwezesha sekta muhimu za uzalishaji na huduma za jamii kushamiri kikiwemo kilimo, nishati, uchumi wa kidigiti, hifadhi ya mazingira, maji, elimu na ujenzi wa wa miundombinu ya usafirishaji.
Bi. Kwakwa aliahidi pia kuwa Benki ya Dunia itashiriki kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Kikanda itakayotekelezwa katika nchi tatu za Tanzania, Burundi na DRC kwa kuwa mradi huo ni muhimu katika kukuza biashara na uwekezaji katika Ukanda mzima wa nchi za Afrika.
Bi. Kwakwa alisema pia kuwa Tanzania ni miongioni mwa nchi 15 zilizochaguliwa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kunufaika na mpango wa biashara ya kuuza hewa ya ukaa duniani ambapo Benki hiyo itatoa fedha za kuimarisha sekta ya misitu ili fedha zitakazopatikana kupitia biashara hiyo ya hewa ya ukaa ziwezekusaidia maendeleo ya nchi.
Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 5.5, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 12.6 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 26 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 21 yenye thamani yad ola za Marekani bilioni 4.804 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.698 ni ya kikanda