Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia leo Jumatano Machi 1, 2023 huku bei ya petrol na dizeli zikipaa ikilinganishwa na Februari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Mwainyekule imesema kuwa kwa Jiji la Dar es Salaam bei ya mafuta ya Petroli itauzwa Sh .2,960 ikilinganishwa na Sh.2,819 ya mweziuliopita wa Februari.
Wakati bei ya petoli ikiuzwa hivyo na bei ya dizeli imeongezeka kidogo kutoka Sh.3,105 Februari hadi Sh.3,130 mwezi huu sawa na ongezeko la Sh.25.
Upande wa dizeli kwenye mikoa hiyo imeshuka kwa Sh.209 kutoka Sh.3,340 Februari hadi Sh.3,131 mwezi huu.
Kwa upande wa mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Mtwara ambayo inahusisha mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) bei ya mafuta ya petroli itaongezeka kwa Sh.138 na ya dizeli itapungua kwa Sh.68.
Hata hivyo kupanda kwa bei hii inakuja baada ya Serikali kuondoa ruzuku ya mafuta ambayo ilikuwa inapunguza ukali wa bei hizo.