Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani
Baraza la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, limelaani vikali kitendo kauli ya Wanawake wa Chadema (BAWACHA) ,Kanda ya Pwani kutangaza kuchoma moto vitenge walivyopatiwa kama zawadi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ,March 8,2023 Siku ya Kongamano la siku ya wanawake Duniani.
Limeeleza Kitendo hiki kimetafsiriwa kama uvunjifu wa amani unaoweza kuhatarisha utulivu wa nchi.
Akiwasilisha tamko hilo, Mwenyekiti wa UWT Mkoani Pwani, Zainab Vullu amesema kuwa wale wanaofanya vitendo hivi ni kama watu wenye macho lakini hawaoni, na wenye masikio lakini hawasikii.
Ameeleza kuwa hawaoni wala kuthamini juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia katika sekta mbalimbali za maendeleo, ikiwemo afya, elimu, maji, kilimo, na uchumi kwa ujumla.
Aidha, Vullu amewahimiza wanawake wa UWT Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa wamoja na kushikamana, huku wakisimama imara kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ilani na kusimamia masuala ya wanawake nchini.
Mnamo Septemba 30 mwaka huu, Bawacha Kanda ya Pwani, wanadai Rais hajatekeleza mambo yao Tisa ikiwemo kuboresha afya kwa akinamama na watoto.
Pia, kupunguza tozo kwa wafanyabiashara wadogo akinamama, kupunguza tatizo la ajira,kushughulikia sheria ya ndoa, na kusimamia matukio ya Utekaji, masuala ambayo yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi hatua kwa hatuaā€¯
Hivyo kutokana na hayo Bawacha wamemua kumaliza hasira yao kwa kuchoma moto vitenge walivyopewa na Rais kama zawadi baada ya wao nao kumpa tuzo ya Demokrasia na maridhiano march 8,2023, maamuzi ambayo yanaonekana kumkosea heshima Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.