Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Sosopi, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni wanachama wa Chadema.

Baadhi ya wanafunzi hao wakifuatilia mkutano huo.

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) limedhamiria kuzunguka nchi nzima kuwahamasisha vijana kudai uhuru wa kujieleza ambao wamedai haupo kwa sasa nchini.

Hayo yalisemwa jana kwenye mkutano wa wanafunzi wanachama wa chama hicho wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliokuwa wakijdili masuala mbalimbali ya kisiasa nchini.

Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa DDC Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Sosopi, alisema Bavicha anayoiongoza siyo ya kulalamika bali ni yakutenda kazi.

Aliendelea kueleza kwamba anasikitishwa kuona vijana wananyimwa uhuru wa kujieleza, akitolea mfano kuwa yeye amekamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kichochezi mara nyingi na kufunguliwa kesi mbalimbali lakini alishinda.