Watoa huduma za dharura wamekuwa wakiwaokoa abiria waliokuwa wamenasa ndani ya basi lililosombwa na mafuriko kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi kaskazini mwa Kenya.
Basi hilo, likiwa na takribani abiria 50, lilikuwa likielekea mji mkuu, Nairobi, kutoka kaskazini mwa kaunti ya Wajir, polisi walisema.
Dereva alikuwa amejaribu kuvuka sehemu ya barabara iliyofurika maji. Basi basi likakwama kwenye tope lililozingirwa na maji yenye nguvu.
Baadhi ya abiria waliokolewa kutoka kwenye paa la gari hilo. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema ilikuwa “operesheni yenye changamoto ya uokoaji” kuokoa maisha ya wale “walioathiriwa na maji yanayoendelea” katika eneo la Lager Areli karibu na kijiji cha Tulla kaunti ya Tana River.
Kisa hicho kilitokea alfajiri ya Jumanne baada ya mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha Barabara kuu ya Garissa-Nairobi kujaa maji.
Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha basi hilo linalomilikiwa na Umma Express likizama kwenye maji ya mafuriko.