Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ifikapo 2025 Serikali haitaagiza sukari nje ya nchi kwani kutakuwa na uzalishaji wa kutosha ndani ya nchi.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dodoma leo Januari 10, 2023, Waziri Bashe amesema lengo la Serikali lilikuwa ni kutoagiza sukari nje ya nchi ifikapo 2030.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

“Malengo ya nchi ni ilikuwa kuwa ifikapo mwaka 2030 uagizaji sukari uwe sifuri lakini kwa mikakati tuliyoiweka nawahakikisha mwaka 2025 itakuwa mwisho “amesisitiza Bashe na kuongeza kuwa.

“Tumegundua tatizo liko wapi,maana mwaka jana zilimwagwa tani za miwa zipatazo laki tatu kisa wakati wa kuvuna miwa inayovunwa kwa mtindo wa ushirika kuna baadhi ya wakulima ambao hawaishi maeneo ya ushirika ulipo mashamba yao hayakuvunwa,lakini mwaka huu zimemwagwa tani 8000 tu,kwa hiyo tumegundua hilo lilikuwa linatupa hasara,” amesema.

Aidha waziri huyo amesema wizara yake itahakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 inapunguza kwa kiasi kikubwa kuagiza bidhaa nyingine kama mafuta ya kula,ngano, mchele zinazoagizwa nje ya nchi .

Katika hatua nyingine amesema mikakati mingine katika wizara hiyo ni kuboresha eneo la uzalishaji wa mbegu bora ili kutosheleza mahitaji ya nchi.

Wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali leo Januari 10,2023 mkoani Dodoma.

Amesema hatua hiyo itaiwezesha nchi kuzalisha kwa tija na hivyo kuifanya nchi kujitosheleza kwa chakula kutokana na uzalishaji wenye tija utakaotokana na mbegu Bora.

Aidha amesema hivi delta ya Kilimo inachangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 26.1 huku akisema sekta hiyo inachangia katika malighafi za viwandani kwa asilimia 65.

Baadhi ya wahariri wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe