Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tanga-

WAZIRI wa Kilimo,.Hussein Bashe (Mb), ametangaza neema katika mradi wa Umwagiliaji Mkomazi uliopo Korogwe mkoani Tanga na kusema ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere inatimizwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya Umwagiliaji Mkoani Tanga, Waziri Bashe ametangaza neema ya kukamilishwa miradi yote ya umwagiliaji.

Amesema, miradi hiyo ya umwagiliaji ukiwemo mradi mkubwa wa Mkomazi wenye gharama zaidi ya bilioni 18.2 ni ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere inayotimizwa serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

Amesema bwawa hilo litahifadhi maji mita za ujazo bilioni 17.5.

Bashe ameongeza kuwa azma ya serikali kutekeleza miradi ya Umwagiliaji katika Bonde la Mkomazi, wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga; kutawasaidia wananchi kuondokana na Umwasikini wa kipato na kuchangia katika pato la taifa.

“Hatua inayochukuliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imetatua changamoto ya muda mrefu ya utekelezaji wa mpango wa kilimo cha Umwagiliaji katika bonde la mkomazi,ambao umekuwa mjadala kwa miaka mingi toka serikali ya awamu ya kwanza,”amesema.

Waziri Bashe amesisiitiza kuwa mabwawa 100 na mabwawa 14 ya vipaumbele ya Rais Dkt. Samia,yanatekelezwa na Mkomazi ni moja wapo hivyo ni lazima likamilike kwa wakati.

Pia,Bashe amekagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa bwawa la umwagiliaji Mangamtindiro, Chekelei, na kuzungumza na wananchi wa skimu ya Chekelei na Manga.

Miradi yote iliyotembelewa ipo katika bonde la Mkomazi, isipokuwa sehemu kubwa ya mradi wa Chekelei ambao upo nje ya bonde hilo.

Katika ziara yake kwenye kata ya Mazinde, yenye zaidi ya watu 14,000, Waziri Bashe alieleza kuwa serikali imeanza mradi wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji lenye thamani ya shilingi bilioni 18, ghala, na mashine ya kukoboa mpunga pamoja na ujenzi wa barabara inayounganisha eneo la mradi na barabara kuu.

“Serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeamua kuwekeza katika kilimo kutimiza ahadi ya muda mrefu kuwa kilimo ni uti wa mgongo,” alisema Bashe. Aliongeza kuwa kupitia ujenzi wa bwawa, wananchi wataweza kuzalisha mazao kwa kipindi cha mwaka mzima.

Waziri Bashe amesisitiza kuwa mashamba yatapimwa na kila mkulima atapewa hati ya kumiliki shamba lake. Serikali inaleta kituo kikubwa cha zana za kilimo ambapo wakulima watalimiwa kila hekari kwa shilingi 40,000 na kituo hicho pia kitakuwa na mbolea za ruzuku na pembejeo zingine.

“Tunamshukuru sana Mungu kwa mara ya kwanza tumepata rais anayehakikisha kuwa keki ya taifa inamfikia hata mkulima,” alisema Bashe.

Ameiagiza Kampuni ya Serikali ya Mbolea (TFC), kuingia makubaliano na wakulima wa Mkomazi na Mazinde na kuanzisha kituo cha mbolea katika maeneo hayo.

Pia amepiga marufuku uuzaji wa mazao kwa lumbesa na kusema unanyonya wakulima hivyo ofisi ya Mkuu wa mkoa ione namna ya kuthibiti