Kwa zaidi ya miezi kumi nchi ya Syria imeingia katika mzozo uliosababisha machafuko makubwa nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 1300 kupoteza maisha. Mzozo huo unasababishwa na wananchi wa nchi hiyo kutoikubali serikali inayongozwa na Rais Bashar al-Assad.

 

Hatua iliyofikiwa katika vita hiyo sasa imesababisha mataifa makubwa na yenye nguvu kichumi na kijeshi  kama Uingereza, Marekani Urusi na China kuingia katika vita hiyo.

 

 

Tayari Marekani imeripotiwa kupeleka meli zake za kivita katika bahari ya Meditrrenian hatua ambayo imepingwa na Urusi na China ambazo zinaripotiwa kumsaidia Rais Assad kwa madai kuwa Syria ilitumia silaha za sumu katika vita hiyo.

Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema tuhuma kuwa Serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali ni upuuzi mtupu.

Amesema Jeshi la Syria lilikuwa linasonga mbele, hapakuwa na sababu ya serikali kuwapa kisingizio wanaotaka kuingia kijeshi.

Putin amesema ikiwa Marekani ina ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zake, basi iukabidhi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Alimkumbusha Rais Barack Obama wa Marekani kuwa aliwahi kutuwa Tuzo ya Amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio.

Alikaribisha uamuzi wa Bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema ameshangazwa na uamuzi huo wa bunge.

Wachambuzi wa mambo ya kivita wanasema hatua ya mataifa haya kuingia katika mzozo huo inaweza kusababaisha vita kuu ya tatu ya Dunia au kurudisha vita baridi baina ya mataifa ya Marekani na Urusi.

Tayari Rais Bashar al-Assad ameionya Marekani iwapo itathubutu kuishambulia Syria atalisambaratisha taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kiuchuni na kijeshi duniani. Amesema harakati za kijeshi zinazoendeshwa na taifa hilo hazitafua dafu.

“Marekani itafeli kama ilivyoshindwa hapo awali katika vita ambavyo walianzisha, kuanzia Vietnam hadi sasa,” amesema.

 

Bashar al-Assad ni nani
Bashar Hafez al-Assad, Rais wa Syria,  alizaliwa Septemba 11, 1965 katika  mji wa Damescus,  Syria.

Baba yake, Hafez al-Assad, alizaliwa katika familia maskini na ndiye aliyefanikiwa kufufua Tawi la Chama cha Kiarabu cha  Kisoshalisti cha  Ba’ath nchini Syria ambapo baada ya mapinduzi ya mwaka 1970 aliingoza nchi hiyo.

Ufanisi  na umakini  wa  Hafez al-Assad  katika historia ya Syria  kama kiongozi ndiyo uliompa jina la Simba katika  mataifa ya Kiarabu.

Alipata elimu ya msingi na sekondari katika  shule yenye mchipuo wa lugha za Kiarabu-Kifaransa  ya Al-Hurriya katika mji wa Damascus

Mwaka 1982 alihitimu sekondari na kwenda kusomEa ufamasia na matibabu katika Chuo Kikuu cha Damascus. Mwaka 1988, Bashar al  Assad alihitimu kozi hiyo na  kufanya kazi kama daktari katika hospitali ya Jeshi “Tishrin” iliyoko nje kidogo ya  mji wa Damascus.

Miaka minne baadaye, alikwenda Uingereza  kuanza mafunzo shahada ya uzamili Kitengo cha  Ophthalmology  katika Hospitali ya Western Eye sehemu ya hospitali za kufundishia za St. Mary jijini London.

Bashar  Al Assad wakati  huo alikuwa hana matarajio makubwa  ya kuwa mwanasiasa ambapo kaka yake, Bassel al-Assad, alitarajiwa kama rais wa baadaye, lakini hakutangaza dhamira hiyo.

Mwaka 1994,  Rais  Bashar  aliitisha kikao cha na jeshi baada ya  kifo cha kushtukiza cha kaka yake,  Bassel kilichosababishwa na ajali ya gari. Muda mfupi baada ya kifo cha Bassel, Hafez Assa, baba wa Rais wa Syria  alimtangaza Bashar Al Assad kama mrithi wa Utawala wake.

Rais Bashar Assad aliandaliwa utaratibu maalum wa kutambulishwa uliokuwa katika awamu tatu. Kwanza alimpeleka jeshini, pili picha yake ilitambulishwa kwa umma na tatu alikaimu madaraka kama kiongozi wa Syria baada ya kifo cha baba yake mwaka 2000.

Baada ya kifo cha baba yake, mwaka 2000 Bashar aliteuliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Ba’ath na Jeshi, na alichaguliwa kuwa rais bila kupingwa katika Bunge la nchi hiyo kwa kupata asilimia 97.2 ya kura.

Sanjali  na kazi yake ya kijeshi, Bashar alikuwa mshiriki mkubwa katika masuala ya umma. Alipewa mamlaka kubwa kama mshauri wa kisiasa kwa Rais Hafez al-Assad, mkuu wa ofisi ya kupokea malalamiko ya rufaa ya wananchi, na pia aliongoza kampeni dhidi ya rushwa.

Mei 27,  2007 Bashar aliapitishwa kama rais kwa kipindi kingine cha miaka saba, pamoja na matokeo rasmi ya asilimia 97.6 ya kura za maoni. Baada ya kushika madarala alibadilisha maisha ya watu wa Syria tofauti ya wakati wa baba yake kisiasa na kiuchumi.

Katika uhusiano wa nje.

 

Bashal al Assad amekuwa na uhusiano wa karibu na mataifa ya China na Urusi kutokana na uwekezaji mkubwa wa mafuta ndani ya nchi yake, lakini pia uhusiano mdogo na uliotetereka kwa jumuiya ya nchi za kiarabu na mataifa ya Magharibi.

 

Kutokana na upepo wa mabadiliko katika mataifa ya kiarabu  ulioanzia Tunisia, Serikali ya rais Bashar  al Assad haikusalimika  katika mabadiliko hayo. Januari 26, 2011 Wasyria waliandamana kupinga uongozi wake.

Wito wa waandamanaji hao ni kutaka mageuzi ya kisiasa  na kurejeshwa kwa haki za kiraia, pamoja na kuondolewa kwa sheria ya hali ya hatari ambayo imedumu tangu mwaka 1963.

 

Bunge la Uingereza

Bunge la Uingereza limepiga kura ya kupinga muswada uliowasilishwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron wa kutaka idhini ya  kuishambulia kijeshi Syria. Baada ya vuta ni kuvute kali iliyotawala kikao hicho, wawakilishi wapatao 285 dhidi ya 272, walipinga muswada huo na hivyo kutoa pigo kali kwa David Cameron.

 

Baada ya kikao hicho, Waziri Mkuu huyo wa Uingereza, amesema kuwa ni wazi kwamba Bunge linapinga hujuma ya kijeshi dhidi ya Syria.
Amesema serikali yake itafuata uamuzi wa Bunge kuhusu kadhia hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Uingereza kupingwa na Bunge kuhusu suala la kwenda vitani tangu mwaka 1782.

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, imeonesha kusikitishwa kwake na mashambulizi tarajiwa ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Syria.

Katika ripoti yake iliyotolewa wiki iliyopita, wizara hiyo imelaani mashambulizi yanayotarajiwa kufanywa na Marekani na rafiki zake dhidi ya Syria na kusema uingiliaji huo hautakuwa na tija yoyote zaidi ya kuwaua raia wasio na hatia na kuharibu miundombinu ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Afrika Kusini imesisitiza kuwa mgogoro wa Syria unapaswa kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia. Aidha, imeonya  kuwa tija ya vita dhidi ya Syria haitabiriki na kwamba itasababisha hali ya mambo kuwa tete zaidi. Kwa upande wake, Gilad Atzmon, mkosoaji maarufu wa Kiyahudi amesema kuwa hivi sasa Rais Obama amechanganyikiwa kuhusiana na kadhia ya Syria.

 

Amesema Obama hataki kuishambulia Syria, lakini yuko chini ya mashinikizo makali ya Wazayuni suala ambalo limemfanya achanganyikiwe na kushindwa kuchukua uamzi sahihi kuhusu suala hilo. Uingereza huenda ikaanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria,bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Mashambulio hayo yatahitajika ikiwa yatatekelezwa ili kuzuia raia kuuawa, hata ikiwa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Urussi na Uchina zikitumia kura zao za turufu kupinga mikakati ya kijeshi dhidi ya utawala wa Syria.

Maafisa wa ujasusi nchini Uingereza wamemueleza Waziri Mkuu, David Cameron, kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Serikali ya Syria ilihusika na shambulio la kemikali wiki iliyopita mjini Damascus.

Serikali ya Syria imekana madai ya kutumia silaha za kemikali katika shambulio mjini Damascus Agosti 21, mwaka huu ambapo mamia ya watu waliuawa.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, imechapisha ripoti kuambatana na ushauri wa mkuu wake wa sheria Dominic Grieve, inayotoa idhini ya mashambulio ya kijeshi ili kuzuia utumiaji wa silaha za kemikali siku zijazo, kuambatana na sheria za kimataifa.

 

Ban Ki-Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema atapokea ripoti kutoka kwa wachunguzi wake wa silaha wanaochunguza ikiwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria.

Rais Obama amesema hajaamua kuhusu mpango wa kuishambulia Syria kijeshi.

 

Mataifa mengine pia yanajadili hatua yak uchukua, na Uingereza imekuwa ikishinikiza Baraza la Usalama la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio litakalohakisha raia wanalindwa nchini Syria.
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema taifa lake litajilinda kutokana na shambulio lolote kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Ed Miliband
Awali Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Labour, nchini Uingereza, Ed Miliband, alisema Bunge la nchi hiyo halipaswi kuamua ikiwa itaidhinisha mzozo wa Syria kutatuliwa kijeshi.

Milliband amesema wamejifunza mengi kutokana na uamuzi uliochukuliwa miaka ya zamani kama ule wa kuivamia Iraq.

Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuipa jopo maalum na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nafasi ya kufanya kazi yao.

 

Mwisho.