Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Kibaha

“Mjitokeze kwa wingi kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura, Natarajia kuona watu sita ndani ya kila saa ili tufikie malengo yetu ya uandikishaji kwa mkoa,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge.

Ili kuhakikisha mafanikio ya zoezi hilo, ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani imeandaa mbio za kuhamasisha wananchi (jogging) kukimbia urefu wa km 5 ambazo zimefanyika Oktoba 12, 2024 katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Maili Moja, Kibaha, Pwani.

Zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani zaidi ya wananchi 1,000 wamejitokeza kushiriki mbio hizo.

Kunenge alieleza kuwa uandikishaji wa wapiga kura unaoendelea kati ya Oktoba 11 na 20, 2024 ni maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Pia aliwashukuru wananchi waliojitokeza tangu zoezi lianze na kuwataka waendelee kujitokeza kwa wingi.

Mkoa wa Pwani una vijiji 417, vitongoji 2,028, mitaa 73, na vituo vya uandikishaji 2,374.

Please follow and like us:
Pin Share