Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasema kikao cha pili cha Baraza la Usalama la ()UN kitafanyika kujadili mgogoro unaoendelea katika mkoa wake wa mashariki.

Mkutano mpya ulioitishwa na viongozi wa Kongo unafuatia mapigano ya kundi la waasi la M23 huko Goma Jumatatu, huku hofu ikiendelea kuongezeka kwamba jiji hilo litaangukia mikononi mwa waasi.

Waziri wa mambo ya nje wa DRC Therese Kayikwamba Wagner alisema hakufurahishwa na taarifa ya Baraza la Usalama la UN iliyotolewa Jumapili, ambayo ilitaka kujiondoa kwa “vikosi vya nchi za nje” kutoka nchi yake ambayo ni tajiri ya madini.

“Serikali yangu inaeleza kufadhaishwa na jinsi Baraza la Usalama limetoa taarifa rahisi, isiyo wazi, na isiyo na maana,” alisema, na kuongeza kuwa Rwanda inahitajika kutambuliwa wazi kama “mshambuliaji.”

Wengine katika DRC wanatumai kuwa machafuko na uharibifu unaosababishwa na kuingia kwa waasi wa M23 katika sehemu za Goma Jumatatu utasukuma Baraza la Usalama la UN kuchukua hatua kali wakati wa mkutano siku ya Jumanne.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika pia litakutana siku hiyo hiyo kujadili hali ilivyo mashariki mwa DRC.