Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mara, leo Jumatano tarehe 23 Aprili 2025, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku tano, mkoani humo.
Ziara ya Balozi Nchimbi mkoani Mara inahusisha pia kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, kupitia miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo, zinazotekelezwa na Serikali ya CCM, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa CCM, katika kuwatumikia wananchi.

Mapema kabla ya kikao hicho cha ndani, Balozi Nchimbi alitembelea na kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Musoma na Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo yote inajengwa mjini Musoma.
Akiwa katika ofisi hizo za CCM Mkoa wa Mara, Balozi Nchimbi pia alipata fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi huo ulioko katika hatua ya ukamilishwaji, ambapo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kutumiwa na watu 2,000 – 2,500 wakiwa wamekaa.





