Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Songea
JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha uhuru wa wanahabari.
Pongezi hizo zimetolewa leo Aprili 4, 2025 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile wakati wa ufunguzi wa mkutano maalum wa TEF unaofanyika Songea mkoani Ruvuma.
“Kwa hakika uhuru wa vyombo vya habari umeimarika ambapo magazeti yaliyokuwa yamefungiwa yamefunguliwa, adhabu na faini zimeondolea au kulegezwa na hofu ya waandishi wa habari imepungua au kundoka kabisa lakini tumebaki na kisiki cha uchumi wa vyombo vya abari usiotabirika.” amesema.
Balile amesema pia TEF inaipongeza Serikali kwa kuanzisha Bodi ya Ithibati ambayo inakwenda kuanzisha Mfuko wa Mafunzo na Baraza Huru la Vyombo vya Habari hatua ambayo itasaidia kukuza vyombo vya habari na kujengea heshima ya kipekee mbele ya jamii.

“Tunaishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuanzisha Bodi ya Ithibati ambayo ilishindikana kuanzishwa katika kipindi cha miaka tisa tangu mwaka 2016.” amesema.
Aidha, Balile amesema Katibu wa CCM Emmanuel Dk Nchimbi amekuwa rafiki na wanahabari na kuomba baadhi ya viongozi ambao wamekuwa hawana ushiriano na wanahabari kubadilika.
Amesema vyombo vya habari vinamchango kubwa katika kukuza demokrasia, uwajibikaji wa viongozi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Hata hivyo tasinia inakabiliwa na changamoto mbalim zikiwemo za uendelevu wa kiuchumi, uhuru wa aandishi wa habari na maslahi ya waandishi wa habari.
“Tunajua serikali inaendelea kuzishughulikia changamoto hizi na tunaimani kwa pamoja tunaweza kubuni mbinu mbalimbali za kuhakikisha vyombo vya habari vinabaki kuwa imara na kutoa huduma bora kwa jamii.
“Ni ukweli ulio wazi kuwa uchumi wa wanahabari ni mgumu kweli tunaomba serikali itupie jicho la huruma kwani vyombo vya abari ni muhimu mnno katika maendeleo ya jamii yetu.”
Balile amesema TEF inajivunia kuwa mstari wa mbele kukuza uwandishi wa habari wa kitaaluma, maadili na unaozingatia weledi.
“Tunaamini uwandishi wa habari wa uchunguzi unaotegemea ushahidi wa kina ni yenzo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji wa maendeleo ya taifa letu.

Pia TEF inaendelea kuhimiza matumizi sahihi ya teknolojia katika majukwaa ya kidigitali kuhakikisha kwamba habari zinazotolewa zinakuwa za kweli sahihi na zenye manufaa kwa jamii yetu.
Amesema TEF inatambua juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya uendeshaji wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya sheria na sera zinazoaathiri sekta ya habari.
“Tunaomba Serikali ya CCM iendelee kushirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa mazingira haya yahakuwa bora zaidi hususani katika uhuru wa vyombo vya habari upatikanaji wa matangazo na sera ya uchumi wa vyombo vaya habari.” amesema.



