Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Babati

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava amesema Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara haijakurupuka bali imejipanga kwa kuwa na miradi yenye viwango.

Hayo amezungumza Julai 16, Mwaka huu wakati alipokua akiagana na Halmashauri ya Wilaya hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Anna Mbogo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa Wilaya hiyo Lazaro Twange, ambapo aliendelea na Halmashauri ya Mji wa Babati.

Mnzava amesema miradi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo ina ubora ambao unakubarika kabisa, na hivyo kuwataka kuendelea kutunza miradi hiyo, iendelee kutoa huduma kwa wananchi kwa muda mrefu ile ambayo imekamilika.

“Na ambayo bado haijakamilika ikamilike kwa wakati ili nayo iweze kutoa huduma kwa wananchi, na hayo ndio mambo ambayo mh. Ris Dkt.Samia Suluhu Hassan anategemea kutoka hapa Babati DC” amesema Mnzava.

Aidha amesema Halmashauri ya Wilaya ya Babati kazi ni nzuri, hivyo ni vema sasa miradi hiyo ikatumza ili iweze kudumu kwa muda mrefu na hatimaye kuweza kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

” Ndugu zangu sasa Babati hapa mambo yote yalikua mazuri kwa hiyo nikianza kuongea moja moja hatutamaliza na kule Babati Mji wanaona kama tunawachelewesha, lakini inabidi wawe wapole kidogo kwasababu naongea na watu ambao kazi tayari tumeshaiona, ila kwa neno moja tu nzuri ni kwamba Babati Dc kazi ni nzuri.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Anna Mbogo amesema Mwenge wa uhuru ulipokua katika Halmashauri hiyo ulikimbizwa katika miradi 7 yenye thamani ya sh.bil.71,243,967,911

Please follow and like us:
Pin Share