Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kuingia katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupata elimu ya masuala ya Uhifadhi, Utalii, maendeleo ya Jamii, ufugaji nyuki, upandaji miti kutoka kwa wataalam wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo katika maonesho ya kimataifa ya 47 yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.