Wakati wa maelezo mafupi ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa waandishi wa habari katika Ikulu ya White House hapo awali, tulimuuliza jinsi mipaka ya Ukraine inaweza kuonekana ikiwa vita vitaisha –

Je ramani zingeonekana kama zilivyokuwa kabla ya 2014?

Akijibu, Trump anasema “hakika inaweza kuonekana kuwa haiwezekani”.

“Walichukua ardhi nyingi na walipigania ardhi hiyo, na walipoteza askari wengi,” rais anasema.

Lakini anaongeza kuwa “baadhi ya ardhi hiyo ingerudi” kwa Ukraine.

Kama ukumbusho, sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine kwa sasa zinakaliwa na Urusi baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake kamili katika nchi hiyo ya Ulaya mashariki.