Mshambuliaji Iddi Kipwagile ameihakikishia timu yake ya Azam kutinga nusu fainali ya kombe la mapinduzi baada ya kuifunga Simba bao 1-0
Kikosi cha Azam FC leo kimeonyesha dhamira yake ya kutaka kutetea ubingwa wa kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Simba, katika mchezo wa hatua ya makundi uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar.
Ushindi huo unaifanya Azam kufikisha pointi 9, na kurudi kileleni mwa kundi A,huku tayari ikiwa imeshamaliza mechi zake nne na kazi imebaki kutafuta timu ya pili itakayoungana na Azam kucheza nusu fainali ya michuano hiyo timu hizo mbili ni kati ya URA yenye pointi saba na Simba iliyopo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne.
Timu hizo zinakutana Jumatatu jioni kwenye uwanja wa Amaan na ili URA iweze kufuzu kwa hatua hiyo ya nusu fainali inahitaji sare tu wakati Simba inalazimika kushinda mchezo huo ili kuwa mshindi wa pili.
Katika mchezo wa jana ambao ulikuwa na ushindani mkubwa Simba walikitawala kipindi cha pili na kuwapoteza Azam ambao walikuwa wakicheza kwa kujihami huku kipa wao Razak Abalora, akifanya kazi kubwa ya kupangua mashuti ya washambuliaji wa Simba.
Katika dakika ya 26 Mzamiru Yasini alipigashuti kali lakini Abalora alipangua na kuwa kona lakini dakika chache baadaye John Bocco alipata nafasi nzuri lakini shuti lake lilishia mikononi mwa kipa huyo ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Katika kipindi cha kwanza Azam walifanya shambulizi moja la hatari katika dakika ya 38 ambapo mshambuliaji wake Barnald Arthur alipata nafasi nzuri lakini alipiga shuti dhaifu lilidakwa na kipa Emmanuel Mseja na hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazija fungana .
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini Azam ndiyo walionekana kujipanga vizuri zaidi baada ya kuhamia kwenye lango la Simba na dakika ya 46 Yahya zaid alipiga shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari ambalo kipa wa Simba Emmanuel Mseja alilipangua na mpira kugonga mwamba wa juu na kisha mpira kutoka nje na kuwa kona ambayo haukuwa na madhara.
Azam waliendelea kulisakama lango la Simba dakika ya 54 Authur alipoteza nafasi ya wazi ya kuifungia Azam bao la kuongoza baada ya kichwa alichikipiga akiwa ambeki na kipa kudakwa vizuri na Mseja.
Hatimaye dhamira ya Azam ilitimia katika dakika ya 59, ambapo shambulizi kali la kustukiza lilihamia kwenye lango la Simba na kiungo frank Domayo aliyekuwa ameingia muda mfupi kuchukua nafasi ya Salmin Hoza alimtengenezea pasi nzuri winga Idd Kipwagile na kufumua shuti kali lililomshinda Mseja na mpira kutinga wavuni.
Bao hilo lilionekana kuwatimu Simba na kuanza kupambana wakitafuta bao la kusawazisha wakati alinzi wa Azam Agrey Moris na Yakub Momohame wakifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti wasiweze kuleta mashara kwenye lango lao.
Kocha Masoud Djuma, baada ya kuona mambo magumu alimtoa beki Asante Kwasi na kumuingiza mshambuliaji Moses Kitandu na baaday alimuingiza Erasto Nyoni kuchukua nafasi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na walibadilisha mfumo na kutumia mipira mirefu.
Mambo yalizidi kuwa magumu kwa kocha huyo aliamua kumtoa Said Ndemla na kumuingiza Laudit Mavugo ambaye hakuweza kuwamsaada mzuri kwa Bocco na kujikuta timu hiyo ikipoteza mchezo huo kwa mara ya puli mfululizo mbele ya Azam .