Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ametembelea na kukagua mradi wa maji Makere na kurudhishwa na Utekelezaji wake na kuuzindua rasmi na kuelekeza sekta ya maji iufanye mradi huu kuwa somo la kujifunzia katika kutekeleza miradi yake.
Mradi huu unahudumia Vijiji vitatu vya Makere, Kalimungoma na Nyangwa. Ujenzi wa mradi huu umekamilika Kwa asilimia 100 na unatoa huduma ya maji kwa wakazi wapato 30,293 wa vijiji tajwa hapo juu.
Mradi huu umejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Water Mission Kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ujenzi wa mradi umegharimu kiasi cha shilingi 1,213,209,200 hadi kukamilika.
Kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki la lita 200,000, ujenzi wa magati 36 & pilot house hold connection for pre paid meter 1, ujenzi wa nyumba ya mitambo & ya kutibia maji, ufungaji wa mitambo ya kutibu maji, ufungaji wa sola paneli 98, ufungaji wa pampu, ulazaji wa bomba mita 14,667 na uchimbaji wa kisima kirefu.
Mbunge Augustine Vuma Hole wa Kasulu Vijijini ameishukuru Serikali pamoja na Shirika la Water Mission kwa kuhakikisha mradi huu unajengwa na kukamilika na kuwaondolea adha wananchi ya upatikanaji wa maji.
Waziri Aweso ameridhiridhishwa na ujenzi wa mradi huu na kumshukuru Mh. Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na kufungua milango wafadhiri kujitokeza na kushirikiana na Serikali kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji na kuhakikisha adhma ya kumtua mama ndoo kichwani inatekelezwa na kutimia.